Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina amewaapisha waandikishaji wa orodha ya wapiga kura mapema jana Oktoba 7 2024.
Msimamizi huyo wa Uchaguzi amewasihi waandikishaji hao wa Orodha ya wapiga kura kwenda kufanya kazi kama timu "Team work"kwa kushirikiana na wasimamizi wasaidizi ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji ili kuweza kutekeleza majukumu ya Uchaguzi ipasavyo.
Pia amewata kuwa waadilifu na wenye nidhamu ya hali ya juu na kuacha tabia za Ulevi katika kipindi hiki Cha Uchaguzi ili wasije wakaharibu zoezi la Uchaguzi.
Amesisitiza waandikishaji hao kuzingatia mafunzo na ikitokea mtu kuna Sehemu hajaelewa ni vyema akawasiliana na Msimamizi na wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata na vijiji ili kazi hiyo ifanyike kwa weledi bila kuvunja kanuni, taratibu na Sheria za Uchaguzi.
"Nina imani sana na ninyi na nina uhakika mtakwenda kusimamia vyema zoezi hili la Uandikishaji, nendeni mkaoneshe weledi, na ubunifu bila kuvunja kanuni, taratibu na Sheria za Uchaguzi" alisema Dkt Mhina.
Ameendelea kusisitiza kuwa zoezi la Uandikishaji litafanyika kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 11/10/2024 hadi tarehe 20/ 10/2024 na vituo vya Uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na vitafungwa saa 12:00 jioni hivyo kila Mwandikishaji afike kituoni saa 1:00 asubuhi kwa ajili ya Maandalizi ya kituo ili ikifika saa 2:00 asubuhi zoezi la uandikishaji lianze rasmi.
Akitoa taarifa ya Vituo vya Uandikishaji Msimamizi huyo wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amesema Uandikishaji utafanyika kwenye vituo 520, vijiji 126, Kata 37 na , Tarafa 4.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Muheza kujitokeza kwenye zoezi la Uandikishaji kuanzia tarehe 11/10/2024 hadi 20/10/2024 na kupiga kura tarehe 27/11/2024.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.