Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2018, Ndugu Charles Francis Kabeho amewapongeza viongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya Muheza kwa kusimamia vyema Miradi ya Maendeleo iliyopitiwa na mwenge leo tarehe 11/10/2018.
“ Nawapongeza viongozi wote wa Halmashauri, akiwemo Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama,Wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumshi wote kwa kusimamia vizuri Miradi iliyopitiwa na Mwenge kwani Miradi yote 5 ni mizuri, imekidhi vigezo na inaridhisha kwani Wilaya zote tulizopita hakuna wilaya iliyofanya vizuri kama wilaya yenu, nasema hongereni sana “alisema Charles.
Akiendelea kutoa pongezi, Kabelo alisema Halmashauri imeweza kutumia Pesa ya Serikali Vizuri iliyopewa baada ya kusomewa taarifa ya Mradi wa Kituo cha afya Mkuzi na Mganga Mkuu wa kituo kuwa Serikali kuu ilitoa kiasi cha Tshs 372,133,384, Halmashauri 3,575700, Michango ya Wananchi 1,835,000, Nguvu za wananchi 4, 130,800, jumla 381,674,883 ambapo kiasi cha Tshs 353674883 kimetumika kujenga wodi ya mama na mtoto, nyumba ya mtumishi, theatre, maabara na mortuary na kiasi cha shilingi 28,000,000 kimebaki kwenye akaunti.
Katika ukaguzi wa vikundi vya wanawake na vijana na mazingira aewapongeza vijana wafyatua matofali na wahifadhi wa mazingira kwa kuotesha miti na kufyatua matofali ya viwango hali iliyopelekea kumshauri mkurugenzi wanunue vifaa vya ujenzi kutoka kwa vijana hao kwa ajili ya kujengea majengo Ya serikali ili kuwatia nguvu kwani ni vijana wachache wenye mawazo na ubunifu mzuri kama wao.
Kwa upande mwingine mkimbiza mwenge Dominick Rweyemamu amewapongeza viongozi wa wilaya muheza kwa kuhamasisha wananchi wa muheza kwa kuhudhuria kwa wingi katika maeneo yote miradi iliyopitiwa na mwenge na eneo la mkesha wa Mwenge uwanja wa jitegemee pia kwa kuwapitisha kwenye miradi mitano mizuri yenye thamani ya shilingi 1,089,058,748.
viongozi mbalimbali wakikimbiza mwenge wa uhuru kuelekea katika kiwanja cha mpira mkuzi | viongozi wa muheza wakiwa katika uwanja wa kupokelea mwenge mkuzi |
|
---|---|---|
![]() |
![]() |
|
![]() |
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.