Jumla ya miche ya miti 600 aina ya Sederea kupandwa katika shamba la Shule ya Msingi Ngarani na Shule ya msingi Kwakifua zilizopo katika kata ya Tingeni Muheza. "Tanzania ya kijani inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya viwanda"
Akizungumza katika Sherehe ya uzinduzi wa siku ya Upandaji Miti Wilaya ya Muheza iliyofanyika Aprili 19, 2018 katika shule hizo, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo amesisitiza miche hiyo ipandwe katika mashamba na maeneo ya shule hizo ili pindi itakapovunwa iweze kuzisaidia shule hizo kujiendesha. Pia amewataka wataalamu wa Halmashauri kuzipatia shule hizo mbegu za zao la muhogo na mazao mengine ya muda mfupi ili kutatua changamoto ya chakula mashuleni kwa lengo la kuboresha elimu ya msingi.
Awali akisoma risala Mbele ya Mgeni rasmi, Afisa Misitu Ndugu Obadia Msemo amesema pamoja na jitihada kubwa za kuhifadhi na kupanda miti ya aina mbalimbali zinazofanyika wilayani hapo, mahitaji ya rasilimali zitokanazo na mazao ya miti ya asili kama vile Mivule, Mikingu na Minyasa na miti ya kupanda kama vile mitiki, mikaratusi, misederea na mikabela na miti mingine muhimu yameongezeka kutokana na ongezeko la viwanda na ukuaji wa soko la mazao hayo.
Ameongeza kwa kusema kuwa miti ya matunda kama vile miembe, mifenesi na minazi pia imekuwa ikishambuliwa kwa kasi kutokana na uhaba wa miti ya mbao. Ili kukabiliana na changamoto ya ongezeko hili la uhitaji tumeendelea kuwahamasisha wananchi kupanda miti ya tiki na sederea kutokana na ukuwaji wake wa haraka na thamani ya mazao yake. Pia wananchi wameendelea kuhamasishwa kupanda miti ya matunda na viungo kupitia kwa maafisa Ugani wa Halmashauri.
Wilaya ya muheza imekuwa ikipanda miti ya matumizi mbalimbali ikiwamo ya mbao, kuni, vyanzo vya maji, vivuli na viungo kama sehemu mojawapo ya utunzaji wa mazingira. Kwa mwaka 2016/2017 jumla ya miti 2,341,181 ilipandwa na kati ya hiyo asilimia 80 (1,872,945) ya miti yote imefanikiwa kukua. kwa mwaka 2017/2018 lengo la upandaji miti kitaifa kwa kila Wilaya ni kupanda jumla ya miti 1,500,000.
Ndugu Obadia alimalizia kwa kuwasisitiza wananchi kwamba kuzilinda na kuzitunda rasilimali za misitu na mazao ni jukumu la kila mmoja wetu na aliwakumbusha kuwa wao ndio mlinzi namba moja wa kulinda mazingira na rasilimali zilizopo.
Sherehe ya maadhimishi hayo pia yalihudhuliwa na Meneja wa Misitu Wilaya Ndugu Rashidi Shekivunge, Meneja wa Misitu Msaidizi Ndugu Jaston Saria, Afisa Mazingira Ndugu Suleiman Gwaje, Afisa maendeleo ya Jamii Bi. Rose Kimaro, Muwakilishi wa Polisi(OCD), muwakilishi wa ofisi ya Takukuru Ndugu Mwezimpya na Muwakilishi wa ofisi ya Usalama.
HABARI KWA PICHA |
||
---|---|---|
|
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza (Wakatikati) akishiriki kupanda mti na mwanafunzi wa shule ya msingi Kwakifua pamoja na Meneja wa Misitu Msaidizi Ndugu Jaston Saria |
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza akimkabidhi Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kwakifua Miche ya Miti ya sederea
|
|
|
|
|
|
|
Afisa Maendeleo ya Jamii Bi Rose kimaro akishirikiana na mwanafunzi katika zoezi la upandaji mche wa mti aina ya sederea
|
|
Wanafunzi wakiwa kandokando ya mashimo ya kupanda miti tayari kwaajili ya zoezi la upandaji miti
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.