Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imefanikiwa kupitishiwa miradi yote nane ya Mwenge iliyokaguliwa, kuwekewa jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2022 hii ni hatua kubwa ukilinganisha na baadhi za Halmashauri za Mkoa wa Tanga ambazo baadhi ya miradi yake ilikataliwa.
Miradi hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.7 ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa nyumba nne za walimu katika Shule ya Sekondari Misozwe ambao umewekewa jiwe la Msingi, Kukabidhi Samani kwa wanafunzi wenye Mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mbaramo ambao fedha zake zimetokana na michango ya Mwenge
Uwekaji jiwe la Msingi katika Ukumbi wa kijamii wa Muheza Comfort uliopo kata ya Mbaramo na Ufunguzi wa Nyumba za watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza uliopo katika Kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga.
Miradi mingine ni mradi wa barabara ya Mkumbi- Muheza Estate iliyopo katika Kijiji cha Tanganyika yenye urefu wa Kilomita moja iliyogharimu Shilingi Milioni 498.54 ambao kwa sasa umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika Juni 10 Mwaka huu na ule mradi wa Maji MIZEMBWE uliopo katika Kijiji cha Pangamlima kata ya MAKOLE.
Kadhalika Mwenge umekagua Klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Chief Mang’enya na Kikundi cha vijana kinachojishughulisha na kuchakata mkonge cha Mkonge Kwanza kilichopo katika kata ya KWEMKABALA.
Aidha amewataka viongozi wa Muheza kuhakikisha wanasimamia na kufanya dosari ndogo ndogo wafanye marekebisho ili utekelezaji wa miradi uweze kufikia viwango vinavyostahili.
Pia amewasihi viongozi wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi kujitathmini, kuacha dharau na kufuata taratibu za kazi zinavyotaka
“lakini na ninyi viongozi nawasihi msimamie kazi kwa weledi ili utekelezahji uweze kufanyika kwa viwango vinavyotakiwa” alisema Nyanzabara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Bulembo amesema amepokea dosari na marekebisho yote na atahakikisha yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili miradi iweze kukamilika katika muda uliopangwa.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.