Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imekopesha fedha kiasi cha Shilingi Milioni 92 kwa vikundi 14 vya Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu, miongoni mwa fedha hizo Shilingi Milioni 32 ni za mapato ya ndani na Milioni 60 ni fedha za marejesho zitokanazo na vikundi vilivyokwishapatiwa mkopo.
Hafla ya kukabidhi Hundi na Pikipiki za wajasiriamali hao imefanyika siku ya ijumaa tarehe 11/02/2022 katika eneo la mikutano ya Halmashauri ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe, Bulembo amewataka wakina mama kutotumia fedha hizo kwa ajili ya kununua madera ya kwendea kwenya shughuli bali wakatumie fedha hizo kwa ajili ya kuongeza kipato katika familia zao.
Aliendelea kutoa rai kwa Vijana kuwa wakatumie fedha hizo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na sio kuongeza wake wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye pia ni Diwani kata ya Tongwe Mhe Erasto Jerome Mhina amewapongeza wajasiriamali kwa kukidhi vigezo vya kupata mikopo na aliwataka warejesha mkopo kwa wakati ili waweze kuongezewa mingine pia kuwezesha kuwapatia mikopo hiyo wanavikundi wengine.
Awali akisoma taarifa ya utoaji Mikopo kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu, afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Muheza Bi Vije Mfaume Ndwanga amesema katika kipindi cha Mwaka huu wa fedha 2021/2022, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imetenga Shilingo Milioni 213 ambayo ni asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi 42 vya wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
Aliendelea kuwa katika awamu hii ya pili ya utoaji mikopo Halmashauri inatoa mikopo kwa vikundi 8, vya wanawake, Vijana 5 na watu wenye ulemavu kikundi kimoja vyenye jumla ya washiriki 100 wakiwemo wanawake 59, Vijana 38 na watu wenye ulemavu 3.
Aliongeza kuwa makundi ya wanawake yamepatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 49, Vijana wakikopeshwa Shilingi Milioni 39 na watu wenye ulemavu wakinufaika na Shilingi Milioni 4.
Aidha mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi vinavyojishughulisha na miradi mbalimbali ya uchakataji mkonge, usafirishaji abiria na mizigo(bodaboda), ufugaji kuku, ununuzi na uuzaji wa samaki, Duka la vyakula, Mama lishe na biashara ya vinywaji ambapo pikipiki 11 za thamani ya Shilingi Milioni 11zenye thamani ya Shilingi Milioni 25 na Hundi ya Milioni 92 zimekabidhiwa kwa wanavikundi.
|
|
|
|
||
Mkuu wa Wilaya Muheza Halima Bulembo akijaribu kuendesha pikipiki mara baada ya zoezi la kukabidhi Hundi na vyombo vya usafirishaji abiria na mizigo kukamilika (mwenye Kilemba cheusi) ni Afisa maendeleo ya jamii Vije Ndwanga na (alievaa suti nyeusi) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Erasto Jerome Mhina. |
|
Mkuu wa Wilaya Muheza (wa katikati) Mhe. Halima Bulembo akikabidhi Hundi kwa vijana (wa kwanza kushoto) ni Katibu tawala Wilaya ya Muheza Bi Desderia Haule, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Erasto Mhina na wa kwanza kulia ni Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Vije Ndwanga na wapili kulia ni kaimu mkurugenzi Muheza Issa Msumari wakishudia makabidhiano hayo yliyofanyika tarehe 11/2/2022 katika eneo la ukumbi wa Halmashauri. |
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.