Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo amesema wilaya ya Muheza imepewa kiasi cha shilingi Milioni 80 kutoka katika mfuko wa fedha za kupambana na ugonjwa wa Corona kwa ajili ya bweni la wanafunzi wenye Mahitaji maalum.
Akitoa shukrani kwa Serikali, Mkuu huyo wa Wilaya ya Muheza amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kutambua kundi hili la watu wenye ulemavu na kuahidi kusimamia vyema fedha hizo ili ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa.
Ameyasema hayo, wakati wa mapokezi ya ziara ya Mlimbwende Miss kiziwi namba 2 Afrika Hadija Kanyama yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mbaramo yenye watoto wenye Mahitaji Maalum.
Akimtaka mlimbwende huyo kuona umuhimu wa mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum amemuomba Miss kiziwi huyo akashawishi namna ya kusaidia kuongeza madarasa na mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wake Mkalimani wa Miss kiziwi Bi. RAFIA KAEZA amesema kupitia nafasi yake anaweza kupambana mpaka mwisho kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapatiwa haki zao.
Katika hatua nyingine amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaficha watoto wenye ulemavu majumbani kwani kwa kufanya hivyo wanawanyima haki zao za msingi.
“Nikiona wazazi wanawaficha watoto viziwi roho inaniuma sana kwani na sisi tuna haki sawa ya kusoma na kupambania maisha yetu, vizwi tunaweza ndio maana hata mimi nimekuwa Miss japo watu walinishangaa sana niliposhinda nafasi ya pili” alisema RAFIA kwa niaba ya Miss Kiziwi HADIJA KANYAMA.
Awali akisoma risala kwa Mlimbwende huyo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlingano SABRINA RAMADHANI ambaye ni mlemavu amemuomba Miss huyo kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu zinazosababisha wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bora.
Shamra shamra za kumpokea Miss Afrika namba 2 | mlimbwende wa Afrika alivyopokelewa katika maeneo ya Majengo shimoni | MISS AFRIKA AKIWASILI SHULE YA MSINGI MBARAMO | MISS HADIJA KANYAMA AKIKABIDHI ZAWADI | PICHANI NI DC MUHEZA AKIWA NA WATU MBALIMBALI | MISS AKIKAGUA MABWENI |
|
|||||
MADEREVA BODABODA, WANAFUNZI NA WANANCHI WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMPOKEA MISS KIZIWI NAMBA 2 KATIKA ENEO LA MAJENGO SHIMONI | MLIMBWENDE Wa afrika namba 2 akipokelewa katika eneo la Majengo Shimoni Wilayani Muheza. | Miss Afrika namba 2 Hadija Kanyama Akiwasili katika Shule ya wanafunzi wenye Mahitaji Maluum MBARAMO | Miss Kiziwi Afrika Hadija Kanyama akikabidhi zawadi kwa watoto wenye mahitaji maalum jana jumatatu tarehe 19/10/2021 katika Shule ya Msingi Mbaramo | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE, HALIMA ABDALLAH BULEMBO (mwenye kilemba cheupe) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi, waandishi wa habari na Miss Afrika namba 2 | MLIMBWENDE AFRIKA HADIJA KANYAMA AKIKAGUA MABWENI YA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM YALIYOPO KATIKA SHULE YA MSINGI MBARAMO |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.