Halamashauri ya Wilaya ya Muheza,Mkoani Tanga imetoa Mikopo kwa Vikundi 74 yenye Thamani ya shilingi Milioni730,itakayowanufaisha Watu 322.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt Jumaa Mhina alisema hayo mwishoni mwa wiki,alipotoa taarifa kwa Waziri wan chi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete.
Dkt Mhina alisema Mikopo hiyo imetolewa kutimiza takwa la kisheria ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri.
Alieleza Halmashauri ilipokea maombi kwa Vikundi 751 vya Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka Kata 37 zilizopo Wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema Mkopo huo utakuwa na thamani ya shilingi Milioni 730 kati ya hizo shilingi Milioni 286 ni mapato ya ndani na shilingi Milioni 444 zinatokana na marejesho.
Dkt Mhina aliahidi kuwa,wataendelea kutoa mkopo kwa Vikundi vyote vilivyokidhi vigezo.
‘Kuweni na Subira mtapata awamu ijayo kadri fedha zitakavyokusanywa,Vikundi ambavyo havijakidhi vigezo vitaendelea kujengewa uwezo viingie katika kundi la kupata mikopo hiyo’alisema.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu,Ridhiwani Kikwete aliwataka Wananchi waliopata mikopo hiyo kuitumia vizuri na kufanya marejesho wenzao wengine wapate,
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’Alisema kutolewa kwa mikopo hiyo kumetokana na Kazi nzuri zilizofanywa na Serikali.
Alisema Miaka iliyopita Halmashauri haikuwa na uwezo wa kutoa mikopo na waliwahi kutoa shilingi Milioni 20.
Mwinjuma aliwataka Wananchi waliopata mikopo hiyo kutumia kwa malengo tarajiwa na wairejeshe kwa kuijengea uwezo Halmashauri katika utoaji mikopo hiyo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.