Makamu wa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia suluhu Hassan leo tarehe 16/3/2021 ametembelea na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji na mradi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza baada ya kuridhishwa na hatua za utekelezaji ilipofikia miradi hiyo.
Akizungumza katika Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza uliopo katika kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga Wilayani humo Mhe, Samia amesema anapongeza jitihada za Wilaya na Halmashauri ya Muheza kwa kujitoa kikamilifu kusimamia mradi huo kwani mpaka sasa huduma za Afya zinatolewa katika Hospitali hiyo.
Vile vile aliwataka viongozi na wananchi wa Muheza kuendelea kuchapa kazi katika mradi huo kuhakikisha majengo mengine 3 yanayotarajiwa kujengwa yanaanzishwa haraka na kukamilika kwa wakati ili kupunguza foleni katika Hospitali TEULE.
Pia ameitaka Halmashauri kuanzisha huduma ya uzalishaji kwa wakina mama wajawazito ili kupunguza changamoto ya wakina mama wakati wa kujifungua
Akitoa mapendekezo, , Mhe. Makamu wa Rais ameshauri juu ya upandaji wa miti ya kivuli katika eneo la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza ili kujikinga na jua linaloweza kuathiri afya ya wasio wagonjwa na waliowagonjwa.
Alipotembelea na kuweka jiwe la Msingi katika Mradi wa maji PONGWE- MUHEZA uliopo katika kijiji cha Muungano kata ya Mlingano uliogharimu fedha kiasi cha shilingi bilioni sita(6) wenye tenki lenye ujazo wa lita 700,000(laki saba) na utakaonufaisha wananchi zaidi ya 40,000 wa Muheza mjini na pembezoni mwa mradi huu ambao kwa sasa uko katika hatua ya usambazaji wa mabomba Mhe. Suluhu amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa TANGA UWASA BW. Geofrey Hilly kuhakikisha wananchi wanapata maji haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TANGA UWASA GEOFREY amesema ndani ya wiki hii atahakikisha wananchi wanapata maji ili kupunguza changamoto ya Maji Wilayani Muheza.
Mhe. Samia suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi | Mama Samia akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa hospitali ya Wilaya. | Mama Samia na viongzi mbalimbali wakikagua ujenzi wa hospitali. | Mama Samia akiangalia maji | Sehemu ya Waheshimiwa madiwani na watumishi | Sehemu ya wananchi walioshiriki katika hafla ya kumpokea Mama Samia |
|
|
||||
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na wananchi katika kitongoji cha Majengo Wilayani Muheza mara baada ya kuwasili akitokea Wilayani Korogwe leo tarehe 16/3/2021. | Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza iliyopo kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga leo tarehe 16/3/2021 . | Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya mawaziri na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya muheza wakitoka kukagua jengo la WAZAZI mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Hospitali. | Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia maji safi na salama mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa maji Pongwe - Muheza uliopo katika kijiji cha MUUNGANO kata ya Mlingano leo tarehe 16/3/2021. | Sehemu ya watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza walioshuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya leo tarehe 16/3/2021. | Sehemu ya Wananchi walioshiriki kumpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Katika eneo la Majengo mara baada ya kuwasili akielekea katika Mradi wa Hospitali ya Muheza leo tarehe 16/3/2021. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.