Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Mhe Hemedi Suleiman Abdallah ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami inayotoka Muheza mjini hadi Tarafa ya Amani ambayo mpaka sasa imefikia umbali wa kilomita saba(7).
Akizungumza katika Kijiji cha Kilomita saba (7) kilichopo katika kata ya Nkumba ambapo mradi huo umeishia kwa sasa , Makamu huyo wa Rais amesema amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kilomita 40 kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kwa wananchi wa Muheza.
Akitaja faida ya barabara hiyo kwa Wananchi wa Tarafa ya Amani, Mhe Suleimani amesema itasaidia kukuza uchumi wa wakazi wa tarafa ya amani kwa kuwa wataweza kusafirisha mazao yao ya chakula na biashara kwa urahisi kutoka Amani kwenda Muheza na Taifa kwa ujumla.
“Serikali awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inawapenda wananchi wake ndio maana inawasogezea huduma karibu wananchi wake, tutaangalia kama kuna uwezekano wa fedha barabara hiyo ikamilishwe kwa kilomita zote 40 kama ilivyokusudiwa ili iwasaidie wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi kwenda sokoni “ alisema Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Aidha amewapongeza viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa, uongozi wa CCM Wilaya Muheza, ofisi ya Mkuu Mkoa pamoja na viongozi wa Wilaya ya Muheza kwa jitihada walizofanya kuhakikisha barabara hiyo ya kiwango cha lami inafikia kilomita saba (7).
Katika tukio linguine aliwataka viongozi wa CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kukipenda na kukithamini chama chao na kwamba mambo yote walioahidi katika kipindi cha kampeni wayatekeleze kwa kuwa chama hicho cha mapinduzi hakisemi uongo kwa wananchi wake.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.