Wanawake Muheza wahamasishwa Kuwekeza Katika sekta ya Viwanda vidogo vidogo ambavyo malighafi zake zinapatikana Zaidi katika wilaya ya Muheza.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Muheza Tarehe 08/03/2018, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo amewasisitiza wanawake wa Wilaya ya Muheza kuwekeza katika sekta ya viwanda ili kujikwamua kiuchumi kwani ndio kipaombele cha Taifa kwa sasa.
“Kwa niaba ya serikali tupo tayari kumsaidia mtu yeyote anayetaka kuwekeza katika sekta ya viwanda” Alisema.
Aidha amewakumbusha wanawake kutumia fursa mbalimbali zitakazojitokeza katika ujenzi wa Bomba la mafuta kujiinua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji, Bi. Luiza mlelwa amesema kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ilifanikiwa kutoa Mkopo wenye thamani ya Milioni 10, Milioni 5 kwa kikundi cha wanawake Boresha Mazingira ambapo walinunua pikipiki ya magurudumu matatu kwaajili ya kuendeleza kazi zao na kuojingezea kipato, na milioni 5 kikundi cha vijana Malihai ambao walinunua mashine ya umeme ya kufyatua matofali.
Amesema kuwa Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa wanawake na vijana waliojiunga katika vikundi vya wanachama watano watano wenye lengo moja la kujiinua kiuchumi.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Bi. Vije Mfaume amesisitiza kuwa Halmashauri itatoa kipaumbele katika utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake vyenye muelekeo wa kujikita katika uwekezaji wa viwanda.
Wanawake walipata fursa ya kufanya mdahalo juu ya nini kifanyike kuimarisha uchumi wa viwanda wilayani Muheza, Mbinu za kimasoko na kupata elimu mbalimbali za Afya ya Jamii, Msaada wa Kisheria, usawa wa kijinsia kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri pamoja na Bw. Juma Yahya msaidizi wa kisheria kutoka katika Asasi isiyo ya Kiserikali(ZIKOSADI).
Katika maadhimisho hayo Wanawake pia walitoa mchango wa Mifuko 5 ya saruji na ahadi ya Mifuko 2 kwaajili ya Ujenzi wa wodi ya kina mama ambayo ujenzi wake unaendelea kufanyika katika Kijiji cha Lusanga A Wilayani.
Maandamano ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Wilayani Muheza.
|
|
Watatu kutoka Kushoto, Mkuu wa Wilaya Muheza akikagua vikundi vya wanawake vya ujasiliamali katika maadhimisho hayo.
|
|
|
|
||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Ya Muheza Mhe. mwanasha Tumbo
Akikabidhiwa Mifuko ya saruji na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya.
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.