Siku moja baada Maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanaasha Rajab Tumbo ameongoza na kuhamasisha wananchi wilayani Muheza kwa kupanda miti aina ya Mikuvukuvu zaidi ya miti mianne imepandwa kwenye vyanzo mbalimbali vya Maji .
Aidha Mkuu wa wilaya alitoa kiasi cha mifuko hamsini ya saruji kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Mgambo iliopo katika kata ya Misalai Tarafa ya Amani.
Shughuli nyingine zilizo fanyika siku hiyo ni Mkuu wa Wiliya kuhitimisha Mafunzo ya Jeshi la Akiba ambapo Wanajeshi wa jeshi hilo wapatao sabini nanne walikula kiapo cha utii mbele ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya,akiwatia moyo Wanajeshi hao Mkuu wa Wilaya ameyataka Makapuni ya Ulinzi waajiri watu wenye sifa.
Akihutubia wananchi wa kata ya Misalai Mkuu wa Wilaya alitoa onyo “ole wake atakae mzuia mtoto kwenda shule” aliendelea kusisitiza watoto wa pelekwe shule kwa wakati , pamoja na mambo mengine aliwahabarisha wananchi wa Muheza kuwa zabuni ya utengenezaji wa barabara ya Muheza Amani imefunguliwa kwa ajili ya kumpata mkadarasi atakae tengeneza barabara hiyo “Serikali ya awamu ya tano chini ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ambapo Muheza leo hii (10/12/2018) zabuni ya barabara ya Muheza Amani imefunguliwa”
Hata hivyo Mkuu wa wilaya amewaomba wananchi kushirikiana na vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa kuwafichua watu wasio itakia mema nchi yetu, akitoa mfano ameeleza kuwa wapo watu wanalima bangi watu hao hawaitakii mema nchi yetu tushirikiane kuwafichua. .Hata hivyo Mkuu wa wilaya amewaomba wananchi kushirikiana na vyombo hivi vya ulinzi na usalama kwa kuwafichua watu wasio itakia mema nchi yetu, akitoa mfano ameeleza kuwa wapo watu wanalima bangi watu hao hawaitakii mema nchi yetu tushirikiane kuwafichua.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo akikagua Paredi ya Jeshi la akiba | Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo akikabidhi mifuko hamsini ya sajuri kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa zahanati ya Mgambo iliyopo kata ya Misalai tarafa ya Amani
|
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo akihutubia Wananchi wa kata ya Misalai
|
Vijana walio hitimu mafunzo ya Jeshi la akiba wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo Mkuu wa wilaya ya Muheza . |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.