Kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara inayoadhimishwa terehe 09 Disemba kila mwaka Wananchi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Muheza kwa ushirikiano mkubwa wamefanya usafi wa Mazingira siku ya jumanne tarehe 06/12/2022 katika maeneo ya stendi kuu ya mabasi,Ofisi ya Halmashauri, pamoja na Ofisi za ujenzi.
Akizungumza katika shughuli hiyo ya ufanyaji usafi kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Ndug. Edward Mgaya amesema kuwa kama raia wa Watanzania na Wanamuheza watambua umuhimu wa Uhuru na kama watumishi wa serikali ni jukumu la kila mmoja kusafisha mazingira yanayowazunguka kila siku, Aidha ametoa wito kwa wananchi wote kuwa wamoja kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru itakayofanuka tarehe 09 disemba mwaka
Aidha Mkuu wa idara ya Utawala na Usimamizi wa Maliasili Watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Bi. Ruth Mwelo amesema kuwa kama watumishi na wananchi wameadhimisha kuelekea siku ya uhuru kwa kufanya usafi kwa ushirikiano na muitikio mkubwa baina ya watumishi na wananchi wote, pia ameeleza kuwa mbali na shughuli za kufanya usafi pia kuelekea maadhimsho ya miaka 61 ya uhuru ndani ya halmashauri ya wilaya ya Muheza kutakuwa na mashindano ya insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, michezo ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa mikono (netball) baina ya watumishi na waheshimiwa madiwani, kupanda miti katika tarafa ya Amani katika maeneo yote ya vyanzo vya maji, pia mnamo siku ya tarehe 9 disemba kutakuwa na mdahalo na mahojiano ya wazee maarufu wa Muheza watakaoleza historia ya nchi yetu.
|
|
|
Askali jeshi la zimamoto na uokoaji wakiwa katika shughuri za kufanya usafi
|
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya muheza ndug. Edward Mgaya akiwa katika shughuri za kufanya usafi
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.