Takribani Vijana 300 Wa kambi ya CCM mkoa wa Tanga washirikiana kujenga hospital ya wilaya muheza baada ya kukosekana kwa hospitali ya wilaya kwani hospital iliyopo inamilikiwa na kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga ijulikanayo kwa jina la (TEULE) ambayo haitoshelezi, hali iliyopelekea wagonjwa wengi kukosa huduma kwa wakati hivyo basi kusafirishwa wilaya nyingine.
Akisoma taarifa ya Ujenzi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Muheza Ndugu Julius Mgeni amesema tangu Wilaya ianzishwe miaka 45 iliyopita haikuwahi kuwa na Hospitali ya Wilaya ya serikali, huduma za kitabibu kwa jamii zinapatikana katika vituo vya afya na Zahanati vijijini, ambapo Wilaya ina vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali 37 ikiwemo vituo vya afya 2 na zahanati 35.
Akiendelea kusoma taarifa hiyo mgeni amesema kwa kushirikiana na taasisi binafsi vipo vituo vya kutolea huduma za afya 12 ikiwemo vituo vya afya 2, zahanati 9 na hospital 1 Teule ambayo inamilikiwa na kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga ambapo kanisa la Anglikana na serikali wameingia mkataba wa kuwapatia wananchi huduma za kitabibu, lakini bado haina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wilaya kwani uwezo wake wa kuhudumia wananchi 1,500 kwa siku hali inayopelekea wagonjwa wenye hali mbaya za kiafya kusafirishwa umbali unaofikia kilomita 72 kwenda Bombo hospitali ya rufaa mkoa wa Tanga.
NaeMbunge wa Wilaya Muheza mhe balozi Adadi Rajabu, aliwashukuru Vijana kwa moyo wa uzalendo waliouonyesha na kuendelea kuwasisitiza wawe mstari wa mbele kushirikiana ili kuleta maendeleo nchini kwani wao ndio chachu ya kujenga mkoa na Taifa kwa Ujumla na aliahidi kuwapatia vijana hao kiasi cha Tshs milioni moja kwa ajili ya kujikimu kununua mahitaji yao kama sabuni na mafuta
Akiendelea na mazungumzo katika uzinduzi wa kambi ya vijana jana, Mhe Rajabu amewasihi wafanye kazi kwa bidii bila kulazimishwa na kutanguliza pesa mbele bali wawe na moyo wa kujitolea kwani kwa kufanya hivyo ndio watakuwa wametumikia taifa kikamilifu. Pia aliahihidi upatikanaji wa vifaa vya ujenzi katika eneo la ujenzi muda wote na amemshukuru Mhe, Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kutoa kiasi cha Tshs bilioni moja kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza.
Kwa upande mwingine Adadi alitoa taarifa kuwa amepata fursa ya kutengenezewa barabara ya kutoka Muheza mjini –Amani kilomita 40, na kilomita 1 kutoka Muheza mjini –Tingeni itawekuwa ya kiwango cha lami Kutoka Serikali kuu.
Nae afisa vijana Muheza ndugu John Kwingwa ameitaka Serikali itambue uwepo wa vijana wa CCM kwa kuwapatia mikopo waweze kununua mashine za kufyatua tofali za ujenzi na watu waweze kununua na kutumia bidhaa za vijana kwa ajili ya kufikia sera ya Tanzania ya Viwanda.
Kawa upande wa Afisa maendeleo ya jamii wilaya bi vije mfaume Ndwanga ameshaur vijana waendelee kuhasishwa ili wawe wenye muelekeo wa viwanda , wajihusishe katika masuala ya ushonaji.
Mhe mbunge Adadi Rajabu akichota zege
|
|
Mhe Mbunge Adadi Rajabu na viongozi wenzake wakielekea kukagua msingi wa jengo la mama na mtoto
|
|
---|---|---|---|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.