Waziri wa Tamisemi Mhe,Selemani Jaffo jana tarehe 7/7/2020 amefanya Ziara Wilayani Muheza katika Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza uliopo katika Kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga ili kujiridhisha na hatua uliofika mradi huo.
Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Tanga na Wilaya ya Muheza Mhe JAFFO amesema lengo la Ziara yake ni kuja kutembelea Mradi huo na kuona kuwa Maagizo aliyoyaacha katika ziara yake iliopita yametekelezwa ipasavyo.
Amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais DKT John Pombe Joseph Magufuli imetoa msaada wa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga majengo 7 ya Hospitali na hivi karibuni milioni 300 zimeongezwa ili kukamilisha mradi huu.
Katika hatua nyingine ametoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu Tumbo ili Mradi ukamilike kabla ya tarehe 30/7/2020.
Akitoa maagizo hayo Jaffo amesema ahakikishe pesa ilioletwa inatumika ipasavyo na kukamilisha mradi , mafundi wasimamiwe ipasavyo vipande vyote ambavyo havijakamilika vimaliziwe.
Pia kasi ya ujenzi iongezwe kwa kuweka na kufuata mikakati ambayo wilaya itakua imejiwekea
WAZIRI JAFFO AKISAINI KITABU CHA WAGENI | MHE, JAFFO AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA MRADI |
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo alievaa suti nyeusi akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuzungumza na viongozi wa Mkoa na Tanga, Watumishi wa Muheza na wananchi, Mwenye hijjab nyeusi ni Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu TUMBO na wa pili kushoto mwenye koti la Jinzi ni Katibu Tawala Wilaya Muheza Desderia Haule. | Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (mwenye suti nyeusi) Mhe Selemani Jaffo akizungumza na Viongozi wa Mikoa , Wilaya Muheza na Wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya uliopo katika Kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.