Wananchi wa Wilaya Muheza wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo wamefanya harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni 2 ya watoto walemavu na yatima jana katika dhifa ya chakula cha wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo zaidi ya shilingi milioni 500 kimechangwa ili kuwasaidia watoto hao kukaa karibu na mazingira ya shule .
Akisoma taarifa ya michango na ahadi Mkuu wa Wilaya Muheza , amesema jumla ya shilingi milioni 537 ziimechangwa ambapo 12,606,00 fedha taslim, 500,650 kapu la mama , 19,133,000 ahadi za fedha , 11,832,000 ahadi za saruji , 1,440,000 ahadi ya mchanga , 9,400,000 vifaa visaidizi, 473,998,959 ahadi za ujenzi wa mabweni , 8,250,000 ahadi za vitanda 10,240,000 mabati ya mabweni 2 na 5,000,000 ahadi ya vifaa mbalimbali.
Nae Asha Suleiman Iddi (mke wa Makamu wa pili wa Rais wa Mapinduzi Zanzibar ) ambae ndie aliekuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ametoa rai kwa jamii kutowaficha watoto walemavu kwani wana haki ya kusoma na kufanya kazi kama watu wengine pia alichangia kiasi cha shilingi milioni 6 na kompyuta 2 ili ziweze kusaidia katika kutatua changamoto mbalimbali kama kuhifadhi takwimu za watoto hao.
Kwa upande wa Naibu Waziri, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi ,vijana ajira na wenye ulemavu Mhe, Stella Ikupa amekemea tabia ya baadhi ya wazazi\walezi kuwanyanyapaa watoto walemavu kwa kuwafanya kitega uchumi ndani ya familia bali wawape haki sawa kama watoto wengine.
“wapo baadhi ya wazazi\ walezi wanatabia ya kuwaanika juani watoto walemavu, kuwa fanya ombaomba na hivyo basi kuwa kitega uchumi cha familia zao . wale wote fikra na tabia kama hizi za kumdhalilisha mlemavu waache mara moja” alisema stella.
Mama Asha suleiman Idd akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu vizuri darasani
|
|
wageni waalikwa wakiwasili katika dhifa ya chakula cha wanafunzi wenye mahitaji maalum
|
---|---|---|
|
||
|
||
|
|
|
|
|
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu bunge, kazi, vijana ajira na wenye ulemavu mhe, Stella Ikupa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa wilaya muheza jana katika dhifa ya chakula cha wanafunzi wenye mahitaji maalum iliyofanyika katika uwanja wa jitegemee
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.