Leo Februari 6, 2025 Wajumbe wa kamati ya lishe Wilaya wakiwemo, Viongozi wa dini, wataalam wa Afya, baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wamefabya kikao cha Robo ya Pili, Oktoba hadi Desemba ambacho kimejadizwli masuala mbalimbali ya lishe ikiwemo kuweka mkakati wa lishe kuwa agenda ya kudumu kwenye vikao vyote ngazi kuanzia ngazi ya kitongoji Kitongoji hadi Wilaya.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe kwa Robo ya Pili, Oktoba hadi Desemba kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
katika kikao hicho, Afisa lishe Wilaya ya Muheza Bi. Emmanuela Lawrence amesema katika kipindi hicho kuna baadhi ya Viashiria hahijafanya vizuri hivyo lishe ikiwa agenda ya kudumu kwenye vikao vya ngazi zote itasaidia kuboresha hali ya Lishe Wilayani humo
Aliendelea kuwa katika kipindi hicho Vituo ya kutolea huduma za afya 32 vya Halmashauri hiyo vimenunua mbao za kupima hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka 5 ili kuboresha hali ya lishe Wilayani humo.
Aidha Kitengo cha lishe cha Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kinaendelea kutoa elimu na mafunzo juu ya afya za lishe, matibabu ya utapiamlo na upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka 5 kwa kutumia mbao za kupima urefu, kuhamasisha ulaji wa chakula shuleni, matumizi ya vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa wakia na mama wajawazito ikiwa ni sanjari na unyonyeshaji maziwa ya mama pekee kwa watoto chini ya miezi 6
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.