Halmashauri ya Wilaya Muheza imetoa kiasi cha Tshs milioni 15 na kuzigawa katika Shule 3 za Msingi,Masuguru, Kwemkabala, na kwalubuye kila shule imegaiwa Tshs mil 5 kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa baada ya kuona idadi ya Wanafunzi kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya vyumba vilivyopo.
Akizungumza katika Mkutano wa Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri jana tarehe 25/10/2018, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Bakari Zuberi Mhando amesema idadi ya Wanafunzi Shule ya Msingi Masuguru ni 1535, vyumba vya Madarasa Shule ya Kwalubuye ina Wanafunzi 191na idadi ya vyumba vya madarasa wakati Shule Ya Msingi kwembabala ni mpya bado haijaanza
Aidha, Mhando amesisitiza juu ya upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi kwamba kila Diwani kwenye kata yake ni lazima ahakikishe kuwa wanafunzi wanapatiwa chakula ili waweze kufaulu vizuri darasani kwani kwa kushinda na njaa ndo kunasababisha wanafunzi kuwa na matokeo mabaya na aliahidi baada ya baraza lile kutembelea shule zote kufanya tathmini kama wanafunzi wanapatiwa Chakula.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Ndugu Nassib Bakari Mmbagga aliwaomba Madiwani washirikiane na watendaji wa kazi za serikali kuhamasisha katika ujenzi wa miundo mbinu ya shule kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
Kwa Upande mwingine Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Bi Aisha Mhando alisoma taarifa ya utekelezaji wa marekebisho ya kanuni za kudumu kuhusiana na taratibu za mawasilisho ya maswali ya Papo kwa Papo na taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata kusema kuwa utaratibu wa awali wa kuwasilisha maswali ya Waheshimiwa Madiwani kwa maandishi umeondolewa hivyo basi utaratibu wa sasa utakuwa kama ifuatavyo;
1)kanuni ya 23 ya kanuni za kudumu za uendeshaji wa Mikutano na shughuli za Halmashauri, 2016 zimefafanua namna ambayo wajumbe wa Halmaashauri wataweza kuuliza maswasli ya papo kwa papo kwamba Halmashauri ya Wilaya itatenga muda wa angalau dakika 30 katika kila Mkutano wa Halmashauri wa kawaida ambapo Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Halmashauri atajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wajumbe kabla kwa shughuli ya kawaida za mkutano wa Halmashauri.
2)Wajumbe ambao watataka kumuuliza Mkurugenzi au Mwenyekiti maswali ya papo kwa papo watatakiwa kujiorodhesha kwanza kwa Mwenyekiti angalau masaa 24 kabla ya Mkutano wa Halmashauri.
3)Mjumbe yeyote ambaye hajajiorodhesha kwa Mwenyekiti ndani ya masaa ishirini na nne atahesabika kuwa amechelewa, na hataruhusiwa kumuuliza Mkurugenzi au Mwenyekiti swali la Papo kwa Papo.
4)Kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo Mwenyekiti atataja majina ya wajumbe waliojiorozesha kuuliza maswali ya papo kwa papo na idadi ya maswali yanayotarajiwa kuulizwa.
5) Mwenyekiti ataweka utaratibu ambao anaona unafaa na kuridhiwa na wajumbe wa namna bora ya kuendesha kipindi cha maswali ya papo kwa papo;
6) Mjumbe hataruhusiwa kuuliza zaidi ya swali moja la papo kwa papo;
7)maeneo ya umuhimu ambayo wajumbe watatakiwa kuuliza maswali ya papo kwa papo ni:-
8) Baada ya kujibiwa kwa swali, muuliza swali atapewa fursa ya kuuliza swali moja tu la ufafanuzi na maswali yatajibiwa bila mjadala.
9) Mwenyekiti atakuwa na uwezo wa kuruhusu au kukataa swali lolote la papo kwa papo ambalo litaonekana linahitaji takwimu au utafiti zaidi au swali ambalo linalenga kumdhalilisha mwenyekiti au Mjumbe yeyote wa baraza na uamuzi wake utakuwa wa mwisho. Mwenyekiti atakuwa na uwezo wa kutokujibu swali la papo kwa papo iwapo swali hilo litaonekana linahitaji takwimu au tafiti zaidi au litaonekana ni swali la kumdhalilisha mwenyewe au mjumbe wa baraza.
10)Mara baada ya muda wa nusu saa kumalizika, kipindi cha maswali ya papo kwa papo kitamalizia na kuruhusu shughuli zingine za kiko kuendelea
NB. Utaratibu wa uwasilishaji wa maswali ya papo kwa papo umehuishwa ambapo sasa swali HALIAWASILISHWA KABLA YA KUULIZWA isipokuwa mjumbe atajiorodhesha kuonesha nia yake ya kuulizwa swali.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.