Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib Mmbaga ametoa wito kwa Vijana, Wanawake na Wenye ulemavu kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili waweze kupewa mikopo kwa ajili ya kuwakwamua kiuchumi ikiwa ni kutimiza takwa la kisheria .
Akitoa taarifa ya mikopo iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya kwa kipindi cha Mwezi Juni, 2020 MMBAGGA amesema kiasi cha Shilingi 116,800,000 kimekopeshwa kwa vikundi 18 , vikundi 11 vya Wanawake vimepatiwa shilingi 55,000,000 na makundi 7 ya vijana yakikopeshwa TZS 61,800,000.
Akiendelea kuwahimiza wananchi wasiogope kuchukua mikopo hiyo Nassib amesema kiasi cha mkopo kinachotolewa na Halmashauri kitarejeshwa bila riba na kinakopeshwa kwa vikundi ambapo wakopaji wanapewa miezi mitatu (3) ya matazamio kabla ya kuanza marejesho.
Pia amewataka wajasiriamali hao kutumia vyema mikopo waliopewa ili ziweze kuwaletea maendeleo badala ya kujipongeza, kwa kununua nguo mpya, kunywa pombe na kuhonga na kuongeza wake wengine.
“Chukueni pesa hizi mkachakalike ili muweze kurejesha kwa wakati muongezewe fedha nyingine, msije mkatoka hapa kina mama mkaona pesa mliopewa ni ya kununulia dera na khanga nzuri na nyinyi vijana pesa hizi sio za kuhonga wala kuongeza mke alisema Murugenzi wa halmashauri ya Wilaya MUheza
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Mafunzo ya wajasiriamali kilichofanyika jana tarehe 2/7/2020 katika Ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) .
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga amewataka wana vikundi kushirikiana kwa karibu ili kutekeleza malengo ya kikundi yatakayopelekea mafanikio chanya katika shughuli zao za kila siku.
Akiyataja malengo ya kukuza uchumi wa wana kikundi yatakayopelekea uboreshaji wa kaya zao Afisa Maendeleo ya jamii ambae ni Mratibu wa VICOBAWilaya Muheza Bi Rose Kimaro amewataka wana vikundi kuwa na Nidhamu ya kutunza fedha, uvumilivu, Ubunifu , kuishi na watu vizuri, Bidii na kujifunza kutokana na makosa.
Kwa upande Mwingine Afisa Biashara Johari aliwaelezea wajasiriamali kuwa mfanyabiashara mdogo yeyote anatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Mjasiriamali ambacho kinapatikana kwa watendaji wa kata na ofisi ya biashara kwa gharama ya shilingi elfu 20 kwa Mwaka.
Akielezea taarifa ya utoaji fedha za vikundi kwenye akaunti Mhasibu wa Mapato Leospick Vutakamba amesema hatua ya kwanza ni kukiri Mapokezi, Kuwa na kitabu cha hundi, kuwe na taarifa ya mapato na matumizi , pesa zote za mauzo zipelekwe Benki , kuwe na Muhtasari wa wanakikundi.
Wajasiriamali wakiwa katika mafunzo mara baada ya kupokea fedha za mkopo kutoka Halmashauri ya Wilaya Muheza. | Afisa Maendeleo ya jamii ambae ni Mratibu wa VICOBA Rose Kimaro akitoa akiwaelimisha vikundi vya ujasiriamlai namna ya kuwa mjasiriamali bora. | Afisa biashara Johari Kaira Akiwaelelezea wana vikundi Umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Mjasiriamali katika biashara zao |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.