Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina jana amekabidhi Vishikwambi 33 kwa Maafisa Mifugo wa Kata ili kuboresha Utendaji kazi wa wataalam hao.
Vishikwambi hivyo vilivyotoka Serikali Kuu vimetolewa kwa maafisa Mifugo hao wa kata kwa lengo la kuwarahisishia kusajili wafugaji waliopo kwenye maeneo yao ili kutoa huduma stahiki ya chanjo dhidi ya Magonjwa yanayoshambuliwa Mifugo yao.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi yakihudhuriwa na Mkurugenzi, Mkuu wa idara ya Kilimo na Mifugo Ndg Edward Mgaya na maafisa Mifugo wa kata Wa Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ametoa rai kwa Wataalam hao kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo visiharibike na kuisababishia Serikali hasara huku akiwataka wakutane baada ya miezi 3 kuona hali ya utunzaji wa Vifaa hivyo.
" Serikali imetoa vitendea kazi hivi ili kuwasaidia kurahisisha kazi zenu hivyo kila mmoja wenu ahakikishe analinda na kukitunza ili vifanye kazi iliyokusudiwa" alisema Dkt Mhina
Akitoa neno la Shukani kwa Serikali Dkt Mhina amesema anashukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri yake vifaa hivyo huku akiahidi kuvisimamia ipasavyo na kuhakikisha vinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na Serikali.
Nae Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Edward Mgaya ameahidi kuwachukulia hatua wale wote watakaotumia Vishikwambi hivyo Kinyume na taratibu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti maafisa hao wa Mifugo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Vishikwambi hivyo vitakavyorahisisha Zoezi la usajili wa Mifugo ambapo hapo walikuwa wakitumia simu zao za mkononi ambazo zilikuwa na Changamoto hivyo kupelekea zoezi la Usajili na Chanjo ya Mifugo dhidi ya Magonjwa kuzorota.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.