Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mhandisi Mwanasha Tumbo jana tarehe 21/4/2021 amezindua wiki ya upandazi miti ambayo kwa kawaida hufanyika April 01 ya kila mwaka ikiwa lengo ni kuwahimiza wananchi kupanda miti ili kujiepusha na athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza katika maisha ya baadae.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mkurumuzi iliyopo katika Kitongoji cha Tanganyika, kata ya Tanganyika Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wapande miti ili iweze kuwaongezea kipato katika kaya zao.
“Rai yangu kwenu wana muheza wenzangu kila mmoja wetu analojukumu la kupata miti na kuisimamia kikamilifu ili iweze kumletea tija katika maisha yake kwani hakuna uhai bila miti, kupanda miti ni kutetea uhai wetu” alisema Mhe Mwanasha.
Akitoa maagizo kwa Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wa Wilaya Muheza amewataka wahakikishe kuwa miti inapandwa katika Shule zote wilayani humo katika kipindi hiki cha Msimu wa Mvua ya Masika.
Aliendelea kuwa kila Mwananchi aliepo Wilayani humo ahakikishe anapanda miti isiyopungua mitano (5) katika kaya yake ili kumsaidia kupata kivuli na kuboresha lishe ya familia yake.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza na Mkuu wa kitengo cha Nyuki Bw. Issa Msumari amesema kupanda miti ni ustaarabu, hivyo basi wananchi wawe na desturi ya kupanda miti kwani ni mojawapo ya alama ya kukumbukwa.
“Tuwe na utamaduni wa kupanda miti itakuja kuwanufaisha wengine, tusiangalie tutavuna nini sasa hivi tuangalie mafanikio ya baadae alise Bw. Msumari.
Awali akisoma taarifa risala kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo Afisa Misitu Wilaya Muheza Obadia Richard Msemo amesema Wilaya Muheza ina jumla ya hekta elfu thelathini na mbili (32,000) za Misitu ya hifadhi iliyochini ya Serikali kuu ambayo pia wananchi wa jirani hushirikishwa kurejeshea miti kwenye misitu hiyo.
Aliongeza kuwa kwa Mwaka huu wa 2021 Wilaya ya Muheza inatarajia kupanda jumla ya Miti Milioni moja na laki tano(1,500,000) ya aina tofauti katika maeneo mbalimbali Wilayani Muheza katika kipindi hiki cha Mvua za Masika.
Kwa upande wake Mhifadhi wa Misitu Msaidizi (TFS) wa Wilaya Muheza Jackson Saria amesema elimu na maelekezo yataendelea kutolewa kwa wananchi juu ya uvunaji endelevu wa mazao ya misitu ya kupandwa na asili ili kuhakikisha uvunaji wa mazao hayo hauleti athari za kimazingira zitakazopelekea uwepo wa jangwa.
MKUU WA WILAYA AKIZUNGUMZA | MKUU WA WILAYA AKIKABIDHI MITI | MKUU WA WILAYA AKIPANDA MTI | MWENYEKITI HALMASHAURI AKIPANDA MTI | KAIMU MKURUGENZI AKIPANDA MITI | WADAU MBALIMBALI WALIOSHIRIKI SIKU YA UZINDUZI WAKIPANDA MITI |
Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa upandaji wa Miti katika Shule ya Sekondari Mkurumuzi jana tarehe 21/4/2021 | Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo(kulia) akimkabidhi Miti Diwani kata ya Tanganyika Mhe Shafii Chewaja mara baada ya kumaliza kikao cha uzinduzi wa upandaji miti jana tarehe 21/4/2020 katika shule ya sekondari Mkurumuzi. | Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo akipanda mti katika eneo la Shule ya Sekondari Mkurumuzi mara baada ya kikao cha uzinduzi kuisha | Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Erasto Jerome Mhina akipanda mti katika eneo la Shule ya Sekondari Mkurumuzi iliyopo katika Kitongoji cha Tanganyika kata ya Tanganyika jana tarehe 21/4/2021. | Kaimu Murugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Issa Msumari akipanda miti katika eneola Shule ya Sekondari Mkurumuzi siku ya Uzinduzi tarehe 21/4/2021. | |
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.