Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo ametoa rai kwa Wazazi wenye Watoto Walemavu kuacha kuwafanyia vitendo vya ukatili kwakuwaficha ndani kutokana na imani potovu.
Bulembo ametoa rai hiyo kwenye hafla ya Chakula cha Mchana na Watoto wenye Ulemavu wa Akili ilikuwa na lengo la kufanya harambee ya Ujenzi wa Bweni la Shule ya Msingi Masuguru kwajili ya Watoto hao.
“Alimesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani imekuwa ikitoa fedha kwajili ya kuhakikisha watoto hao wanapatiwa Malezi bora ikiwemo elimu hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuwaficha na tukibaini kuwa yupo Mzazi anafanya vitendo vya ukatili dhidi ya motto huyo Serikali itachukuwa hatua kali dhidi yake” Bulembo
Awali Mwakilishi wa Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Issa Msumari amewaomba Wazazi wa Kiume kushirikiana na Wazazi wake katika kutoa huduma kwa Mtoto mwenye Ulemavu na kuachana na imani potovu ambazo zimekuwa zikiwakandamiza Wanawake kwakuonekana ndio chanzo cha kupata Mtoto Mlemavu.
“Alisema Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika mara mama anapojifungua Mtoto mwenye ulemavu na kuonekana kuwa yeye ndio tatizo la kuzaliwa Mtoto mwenye ulemavu hivyo jamii hususa Wakina baba wanapaswa kushirikiana katika kumlea Mtoto huyo na sio kumuachia Mama katika kumuhudumia “Msumari.
Aidha Afisa Elimu Elimu Maalumu Wilaya ya Muheza Muumin Sudi ambae ndio Mratibu wa hafla hiyo amesema Lengo nikutaka kuwaonyesha jamii kuwa Watoto hao wakiwezeshwa wanaweza hivyo Wadau wanayo nafasi ya kuendelea kuwasaidia ili waweze kufikisha Malengo yao.
“Alisema Wamekuwa wakiwafundisha vitu mbalimbali ikiwemo kujitambua hivyo jamii inapaswa kuwapatia ushirikiano ili kuweza kupata furaha kwakujisikia kuwa nao wanathaminiwa hivyo kwakuchangia Ujenzi wa Mabweni hayo itasaidia kuendelea kutoa huduma” Muumin.
Nae Meneja wa Bank ya NMB Wilaya ya Muheza Anna Chimalilo licha ya Michango ambayo wamekuwa wakitoa katika kuwasaodia Watoto hao bado amehaidi kumfungulia Mtoto Akaunt na kumuwekea elf 30 kila mwezi lengo likiwa ni kumuwezesha kupata mahitaji yake ya shule.
|
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo akizungumza na Wazazi pamoja na Wadau wa Maendeleo juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wenye ulemavu
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kwenye Picha ya pamoja na Watoto wenye ulemavu walioshiriki Mashindano ya Umiss
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo akiwa katika Picha ya pamoja na Watoto wenye ulemavu na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kukabidhi zawadi kwa Mshidi wa Umiss.
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.