Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo jana tarehe 23/6/2021 alikabidiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Rajab Tumbo ambaye aliteuliwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 29/5/2021 kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muheza na kushuhudiwa na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, Kamati ya fedha Uongozi na Mipango, wadau wa maendeleo na baadhi ya wana Kikundi cha mazoezi(MUHEZA JOGGING).
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Bulembo amesisitiza ushirikiano katika masuala mbalimbali yaliyopo katika Wilaya ya Muheza ili kuweza kuiletea maendeleo Wilaya ya Muheza.
“kwa kuwa mimi ni mgeni naomba ushirikiano ili kuhakikisha tunapata Muheza tunayoitaka, tukosoane, tueleweshane kwa pamoja, kila mtu afanye kazi kwa bidii katika nafasi yake ilia ache alama” alisema Mkuu wa Wilaya ya Muheza.
Akitoa neno la shukrani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Mwanasha Tumbo amesema anawashukuru viongozi n wananchi wote wa Muheza kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi cha uongozi wake na kuwataka waendelee kumpatia Mhe Mkuu wa Wilaya mpya ushirikiano huo ili kujenga Muheza yenye mafanikio.
“Tulikuwa tunakesha kwa pamoja kuhakikisha jambo letu linafanikiwa, ninachowaomba ushirikiano mlionipa uleule mumpatie Mhe Halima kila mtu kwa nafasi yake ampatie ushirikiano ili kuiletea Muheza Maendeleo” alisema Mhe Mwanasha.
MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO (KUSHOTO) AKIKABIDHIWA OFISI NA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA HIYO MH. MWANASHA TUMBO(KULIA) | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO (KUSHOTO) AKIWA NA MHE. MWANASHA TUMBO ALIYEKUWA DC MUHEZA WAKISAINI KITABU CHA MAKABIDHIANO JANA TAREHE 23/6/2021 KATIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA. | SEHEMU YA WAHESHIMIWA MADIWANI NA WATAALAM WA KAMATI YA FEDHA WALIOSHIRIKI KATIKA MAKABIDHIANO YA OFISI JANA TAREHE 23/6/202021 KATIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA | WAJUMBE KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WALIOSHIRIKI MAKABIDHIANO | WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA WILAYA WAKIKABIDHI ZAWADI KWA MKUU WA WILAYA WA ZAMANI MHE MWANASHA TUMBO | WAJUMBE KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKIKABIDHI ZAWADI KWA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA MUHEZA MWANASHA TUMBO | WAHESHIMIWA MADIWANI KAMATI YA FEDHA WAKIKABIDHI ZAWADI KWA MHE, MWANASHA. | WAJUMBE KAMATI YA WATAALAM WAKIKABIDHI ZAWADI KWA MHE. MWANASHA TUMBO. | WADAU MBALIMBALI WAKIKABIDHI ZAWADI KWA MHE MWANASHA | MHE.MWANASHA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI NA WADAU MBALIMBALI WA WILAYA YA MUHEZA |
|
|
|
|
|
|
|
|||
|
|
|
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.