Katibu Tawala Wilaya Muheza Bi Desderia Haule Nguza ambaye alikuwa Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Muheza Mwanasha Tumbo amefungua Mafunzo ya siku moja ya viongozi wa mabaraza ya kata yaliyokuwa na Washiriki 111 ambapo watendaji wa kata 37, wenyeviti wa mabaraza 37 na makatibu 37.
Hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo ilifanyika mnamo jana siku ya ijumaa tarehe 13/11/2020 katika ukumbi wa mikutano wa walimu (CWT).
Akizungumza katika hafla hiyo Bi Desderia amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu viogozi wanaosimamia kero za wananchi ili waweze waweze kuzitatua
Vilevile kuwawezesha kuwawezesha viongozi hao kutambua vyema namna ya kutenda haki ili waweze kupunguza malalamiko katika jamii.
“Niwaombe viongozi wa mabaraza ya kata Elimu mtakayoipata ikawasaidie kusikiliza kutenda haki na kutatua kero za wananchi kwani miongomi mwenu mmekuwa chanzo cha ongezeko la migogoro kwa wananchi, lakini pia natoa wito kwa wananchi waitumie wiki hii kupata elimu ya kisheria ambayo itawasaidia kufanya maamuzi mbalimbali” alisema Bi Desderia .
Aliongeza kuwa kwa kuwa hapo awali viongozi wa mabaraza hawakuwa na elimu ya ya kutosha ilipelekea baadhi yao kushindwa kuendesha kesi, Hatimaye baadhi ya viongozi walikuwa sehemu ya kuongeza migogoro katika jamii.
Kwa upande wake Muwezeshaji kutoka katika Taasisi ya Tanganyika Law Society Ndugu Charles Livingstone Aro amezitaja sheria 3 za Mirathi kama Sheria ya Mila, Sheria ya Kiislam na Sheria ya kiserikali.
Akielezea sheria ya mirathi ya kimila Charles amesema sheria hii hutoa mamlaka upande wa kiume kurithi mali pale itakapotokea mke au mume amefariki ambapo mali zote zitakwenda upande wa mwanaume hata kama aliefariki akiwa mke katika familia hiyo.
Wakati sheria ya kiislam humpatia mjane moja ya nane ya mali zilizoachwa na marehemu, ambapo wazazi wa marehemu hupatiwa moja ya sita ya mali na kiasi cha mali kilichobaki hupatiwa watoto wa kiume na kike.
Aliendelea kufafanua kuwa sheria ya kiserikali mgawanyo wa mali hufanyika kwa pande zote , ndugu wa marehemu, watoto wote wan je ya ndoa na walio ndani ya ndoa hugawanywa mali ya marehemu kutokana na sheria ya mtoto.
Nae Kaimu Msajili wa Msaada wa Kisheria Wilaya Muheza Herieth Nyangasa amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la siku 3 la uzinduzi wa wiki ya sheria litakalfanyika kuanzia tarehe 17/11/2020 hadi 19/11/2020 ambayo ndio siku ya kilele
Aliendelea kufafanua kuwa baada ya uzinduzi itatolewaelimu ya Mirathi na Wosia kwa wananchi watakaofika katika eneo la soko la zamani la samaki kwa siku hizo , na kuendelea kuwasisitiza wafike ili wakatatuliwe matatizo yao.
ATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA BI DESDERIA HAULE NGUZA AKIZUNGUMZA WAKATI AKIFUNGUA MAFUNZO | KATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA BI DESDERIA HAULE(ALIEBEBA MKOBA) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAWEZESHAJI WA MAFUNZO( WA KWANZA KUSHOTO) NI REGIS KIVALI MWAKILISHI KUTOKA UNDP, WA PILI NI FRIDAH MWAKASYUKA KUTOKA UNDP, WA KWANZA KULIA NI CHARLES LIVINGSTONE, ALIYEVAA FLANA NI ERICK AKARO NA WA TATU KUTOKA KUSHOTO ( PICHA YA MWISHO) NI KAIMU MSAJILI MSAADA WA KISHERIA WILAYA MUHEZA HERIETH NYANGASA | PICHANI NI WANASHERIA WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA, KUSHOTO NI JULIUS NGULIZI NA KULIA NI SIGSIBETH AKWILINI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MADA ZINAZOTOLEWA KATIKA MAFUNZO YA VIONGOZI WA MABARAZA YA KATA | SEHEMU YA VIONGOZI WA MABARAZA YA KATA , WENYEVITI, MAKATIBU NA WATENDAJI WA KATA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAFUNZO |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.