Kamati ya wataalam ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza (CMT) imetembelea miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kukimbizwa Wilayani humo mnamo Mwezi Mei 2022 ili kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika miradi hiyo.
Ukaguzi huo umefanyika ijumaa tarehe 4/3/2022 katika mradi wa nyumba 4 za walimu shule ya Sekondari Misozwe, ambao uko katika hatua ya umaliziaji, ujenzi wa kituo cha afya kwafungo jingo la maabara na wagonjwa wa nje yamekamilika, vyumba 3 vya madarasa na 2 vya tozo Shule ya sekondari Chief Mang’enya vimekamilika, ujenzi wa barabara kilomita 1 MKUMBI- MUHEZA ESTATE iko katika hatua ya uchongaji, vyumba 4 vya Madarasa Sekondari Kwemkabala vimekamilika, mradi wa Maji MIZEMBWE uliopo katika kijiji cha Pangamlima na vyumba 2 vya madarasa Shule ya Msingi Mbaramo uliochangiwa na Mwenge wa uhuru umekamilika.
Baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo kamati imeshauri kufanyiwa usafi kmiradi hiyo na pale amabapo miradi haijakamilika na fedha zipo wamependekeza kuongeza kasi ya ujenzi katika miradi hiyo.
Aidha wameshauri ufanyika ukarabati katika mradi wa matundu ya vyoo 18uliopo katika kata ya kicheba uliofadhiliwa na mjerumani JOSEPH VOGTZ ili kuepukana na athari ya majengo inayoweza kujitokeza katika siku za usoni.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.