Chama cha ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa (CHAWAMU) kimemkabidhi Mkuu WaWilaya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo mifuko 50 ya saruji leo tarehe 20/2/2019 kwa ajili ya kusaidia katika ujenzi wa Hospitalia ya wilaya.
Akisoma Historia ya Chama , kaimu katibu wa chama cha wafugaji wa ng’ombe wa maziwa (CHAWAMU) Bi Zuhura Malenge amesema chama hicho kilianzishwa kisheria mwaka 1993 na kusjiliwa 1994 chini ya mamlaka husika ya ushirika. Na kazi za chama hiki ni pamoja na kutoa huduma ya maziwa, kuchangia mwenge , kusaidia katika shughuli za kijamii kwani walichimba kisima cha Genge pia walichangia pesa ya maafa kiasi cha laki tano .
Nae Mkuu wa Wilaya Muheza Muheza aliwashukuru na kuwapongeza wana Chama wa CHAWAMU Kwa kushirikiana vyema na serikali kwani wameweza kutekeleza ahadi yao walioitoa siku ya harambee na akasema hana cha kuwalipa bali watalipwa na mungu.
“Napenda kuwashukuru wanachama wa chawamu kwa juhudi na mapenzi ya dhati katika kuisaidia Wilaya ya Muheza sina cha kuwalipa mtalipwa na mwenyezi mungu” alisema Mwanasha.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya fedha uongozi na mipango wakifurahia kupokea mifuko 50 ya saruji |
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.