Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 200 kwa Wilaya ya Muheza yenye thamani ya Shilingi Milioni nane (8,000,000) kwa ajili ya kusaidia katika ujenzi wa Shule nne za Msingi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Dismas Prosper kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kwenye halfa fupi iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kilulu alisema kuwa Taasisi hiyo ya kifedha katika Mwaka huu wa 2022 imetenga zaidi ya Bilioni mbili kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali hapa Nchini kote ikiwemo sekta ya Afya, Elimu ambavyo vitanufaika na vifaa kwa Mwaka huu na endapo kutaibuka majanga Benki ya NMB itasimama pamoja na wahanga katika kipindi hicho.
“Pamoja na makubwa yanayofanywa na Serikali wao kama wadau wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kwa kusaidia jamii zetu ndio imefanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko Benki yoyote nchini kuwa Benki ya NMB ndio Benki inayoongoza nchini huku ikiwa na Matawi 226, Mashine za ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB wakala zaidi ya 10,000 na idadi ya wateja zaidi ya Milioni 4 na imefikia kote nchini kwa asilimia 100’ alisema Meneja Prosper.
Pia Meneja kanda Kaskazini Dismas Prosper alisema kuwa Benki ya NMB imetenga fedha kwa ajili ya kusomesha watoto 200 kutoka kwenye kaya duni, Wanafunzi 50 wa Vyuo vikuu na wanafunzi 150 wa kidato cha nne ambao wote watalipiwa Ada pamoja na kupatiwa mahitaji yote ya ambayo yanahitajika katika kipindi chote cha masomoyao Benki ya NMB imekuwa mtari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yao kwa jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Wilaya ya Muheza Anna Chimalilo alisema kuwa Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 200 kwa Shule ya Msingi, Kwakibuyu bati 50, Shule ya Msingi Mtindiro bati 50, Shule ya Msingi Kilulu bati 50 na Shule ya Msingi Bwitini bati 50, Mafanikio hayo yamekuja kufutia kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa Wilaya ya Muheza kuomba kusaidiwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Muheza ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo alisema kuwa anamshukuru Meneja wa Benki ya NMB tawi la Muheza Anna Chimalilo kwa kuwa bega kwa bega kwa kuisaidia Serikali kwa kila jambo linalohusu jamii kuchangia na kufika sehemu ya tukio ambapo ameomba wadau wengine kuiga mfano wa taasisi hiyoya kifedha ambayo imekuwa.
Aliongeza kuwa Waheshimiwa madiwani na walimu ambao wamenufaika na msaada huo kwenda kusimamia bati hizo ambazo wamepatiwa ili kufikia adhima ya kusaidia sekta tya Elimu
“Niwaombe Wahe. Madiwani na walimu ambao mmenufaika na msaada wa mabati kwenda kusimamia vizuri ujenzi na kuezeka mabati hayo katika madarasa huku akiahidi kutembelea kwa ajili ya kukagua ujenzi huo kama umekwenda vizuri” Mkuu wa Wilaya Bulembo alisema.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Erasto Mhina alisema kuwa anaishukuru Benki hiyo kwa kitendo cha kutoa msaada wa mabati ambayo yanakwenda kuboresha elimu hivyo watakwenda kuyatumia vizuri ambapo ametumia hafla hiyo kuwasilisha maombi mawili kwa Benki ya NMB moja ni kusaidia kompyuta na Mashine ya kudurufu karatasi(photocopy)
Mashine kwa ajili ya kutengeneza kituo cha kuchapisha Mitihani kwenye Shule zote za Muheza kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na ombi la pili ni kusaidia ukarabatiwa Shule ya Magila ambayo imekuwa chakavu kutokana na historia kubwa zaidi ya miaka 100 lakini Shule hiyo ina hali mbaya sana kama kuna uwezekano waangalie kwa jicho la huruma sana.
|
|
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe Erasto Jerome Mhina akisisitiza jambo katika hafla hiyo | Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Muheza akizungumza wakati wa makabidhiano | Meneja wa Benki NMB tawi la Muheza Anna Chimalilo akizungumza wakati wa hafla hiyo |
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.