Saturday 23rd, November 2024
@KITUO CHA AFYA MKUZI
Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani hufanyika Agosti 1 hadi 7 ya Mwaka, ikiwa lengo ni kukutana na kukumbushana umuhimu wa unyonyeshaji Maziwa ya Mama pekee kwa mtoto kwa muda wa miezi 6 mfululizo bila kupatiwa chakula chocote cha ziada.
Kuendelea kuongeza uelewa kwa jamii kuwa mtoto anatakiwa kuanza kupatiwa chakula cha ziada kuanzia miezi 6 na kuendelea na kuachishwa kunyonyeshwa pindi afikiapo umri wa miaka miwili(2) ili aweze kuwa na uchangamshi na uelewa wa haraka shuleni.
Kaulimbiu ya Wiki ya Unyonyshaji ya Mwaka huu 2021 “Kulinda Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama wajibu wetu sote” ikiwa na maana kuwa kila mtu kwa nafasi yake katika jamii ana jukumu la kumkumbusha mama kunyonyesha mtoto miezi 6 bila kumpatia chakula chochote.
Kilele cha Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Wilayani Muheza yatafanyika tarehe 6/8/2021 katika kituo cha Afya Mkuzi kilichopo katika kijiji cha Mkuzi kata ya Mkuzi kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo ambae ataongoza hafla hii.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.