Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewashukuru wadau wote wa maendeleo waliofanikisha kupigania maendeleo ya Wilaya hiyo katika kipindi cha Miaka 5 iliyopita cha Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkuu huyo ametoa shukrani hizo jana tarehe 3/12/2020 kwenye sherehe fupi ya Utowaji Vyeti vya shukran na pongezi kwa Wadau wa Maendeleo Walioshiriki kumuunga Mkono Rais Dkt, John Pombe Magufuri katika kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi wake kilichoanzia Mwaka 2015 hadi 2020.
Hafla ya kukabidhi vyeti kwa wadau hao wa maendeleo Pamoja na kukabidhi vyeti kwa jeshi la akiba waliohitimu mafunzo yao kwa kipindi cha miezi 6 kilichoanzia July 01, 2020 imefanyika katika Uwanja wa Jitegemee uliopo katika kitongoji cha Tanganyika kata ya Tanganyika Wilayani Muheza.
Akizuungumza katika hafla hiyo Mhe, Mwanasha Amesema zaidi ya vyeti 400(mia nne) vitatolewa kwa wadau wa maendeleo wakiwemo waandishi wa habari, vyama vya siasa, Taasisi za dini, taasisi za Elimu, Asasi zinazojishughulisha na masuala mbalimbali Wilayani Muheza, Wazabuni,Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza, Wazee, watu binafsi, watoa huduma za burudani na Jeshi la akiba(Mgambo).
Katika hatua nyigine alitoa wito kwa wawekezaji kwenda kuwekeza katikaWilaya ya Muheza katika mazao ya MKONGE na MAZAO YA VIUNGO na kuwahakikishia kuwa maeneo yapo ya kutosha.
Vile vile aliwataka wananchi na wazazi washirikiane kujenga vyumba 3 vya madarasa kila Shule ili kupunguza msongamano wa wanafunzi mashuleni ikiwa ni moja ya kipaumbele cha Wilaya hiyo.
Awali akisoma Taarifa ya Jeshi la akiba Mshauri wa Jeshi la akiba Wilaya ya Muheza Luteni Kanali Charles Madeghe amesema waliohitimu mafunzo ni vijana 66(sitini na sita) wakiwemo wanawake kumi na moja(11) na wanaume hamsini na tano (55).
Aliendelea kuwa mafunzo hayo yalihusisha masomo ya darasani ikiwemo, silaha ndogongogo, mbinu za kivita, ujana pori, ramani, usalama wa raia, Takukuru, huduma za afya, uhamiaji, zimamoto kadhalika na masomo ya nje ya darasa kama kwata, shabaha na mbinu za kivita ambavyo vilifanyika kwa ustadi mkubwa.
Aidha Idadi ya Vijana wa Jeshi la akiba walipoanza mafunzo walikuwa tisini na tatu (93) ambapo wanawake walikuwa kumi na tatu(13) na wanaume themanini(80) ikiwa vijana ishirini na saba (27) walishindwa kuhitimu kwasababu ya utoro.
MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE, MWANASHA TUMBO AKIZUNGUMZA KABLA YA KUKABIDHI VYETI KWA WADAU. | VIJANA WA JESHI LA AKIBAWALIOHITIMU MAFUNZO YA JESHI YA KIPINDI CHA MIEZI 6 | MKUU WA WILAYA MUHEZA MWANASHA TUMBO (KULIA) AKIKABIDHI VYETI KWA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO. | SEHEMU YA WANANCHI MADIWANI WALIOSHIRIKI KATIKA HAFLA HIYO. | BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA TANGA WALIOSHIRIKI KATIKA HAFLA HIYO | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHANDISI MWANASHA TUMBO(MWENYE HIJJAB NYEUSI WALIOKAA) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI |
|
|||||
|
|
|
|||
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.