Katika mahafari ya Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mtakatifu Agustine (SAMIHAS) kilichopo katika Hospitali ya Muheza yaliyofanyika Tarehe 14/2/2025 Serikali imesema mpango wa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii utapunguza mzigo mkubwa katika sekta ya Afya nchi kwa aslimia 52
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza Dkt Fani Mussa alisema kuwa baada ya wahudumu hao kupata mafunzo watawafikia wananchi majumbani kwa kuwa bado wapo wagonjwa wanaotembea umbali mrefu kufuata Huduma za Afya
Pia alisema kuwa mafunzo hayo yameongeza wigo wa huduma zinazotolewa na wahudumu wa Afya ngazi ya jamii mbapo kwa sasa wataanza kutekeleza hatua za kinga na tiba kwa kuwabaini wagonjwa katika hatua ya awali
Aidha alisema watakapohitimu mafunzo ya vitendo na kuanza kutekeleza majukumu yao, wazingatie nidhamu,kujituma, weledi na kutunza siri za wagonjwa na wananchi kwa kuwa kazi yoyote inahitaji nidhamu ‘’Tusitarajie ukiukwaji wa maadili mtakapoanza kazi zenu’’
Dkt Mussa aliendelea kwa kusema kuwa mradi huu jumuishi umetumia kiasi cha zaidi ya billioni 800 kwa kipindi cha miaka 5 amabapo kwa mwaka wa kwanza ilitoa shilingi 99.678 na kwa mwaka 2024/2025 ulianza kwa Halmashauri 23 Mikoa 11
Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Wilayani Muheza Dkt Boniface Pima alisema washiriki waliochaguliwa katika chuo hicho walikuwa 71 na waliofanikiwa kujiunga na mafunzo ni 64
Kwa upande wao wahitimu walisema kupitia mpango wa Afya ya jamii watakuwa na jukumu la kuelimisha jamii kuhusu Afya ilikupunguza maradhi,vifo kuongeza maarifa ya mtu binafsi na jamii
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.