Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Muheza Mkoani Tanga Johari Mtango amewaomba Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuunga Mkono ajenda ya kuomba kupatiwa Halmashauri ya Mji wa Muheza nasio kuendelea kubakia kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akitoa taarifa kwenye kikao cha Ufunguzi wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Muheza amesema tayari hatua mbalimbali zimefanywa kuazia Mwaka 2007 hivyo kuna umuhimu Mkubwa kushirikiana na Wataalamu kwenye ajenda ya kupata Halmashauri ya pili ndani ya Wilaya ya Muheza.
Awali Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo ambae ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masuguru Kombo Dafa alipokuwa akizindua baraza hilo amewaomba Wenyeviti kuhakikisha wanasimamia dhamana ambayo wamepatiwa na Wananchi katika kusimamia Miradi ya Maendeleo ambayo imekuwa ikitekelezwa kwenye Maeneo kwa lengo la kuwasaidia Wananchi.
Nae Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza Ajuaye Msigala amewaomba Wenyeviti wa Serikali na Watumishi wa Serikali kuhakikisha wanatoa elimu kwa Wananchi umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga kura ambalo linatarajia kuaza tarehe 13 ya Mwezi huu.
Aidha kikao hicho cha baraza kilianza na kufanya uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Muheza na Makamu Mwenyekiti ambapo Wajumbe walimchagua Kombo Dafa kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji kwa Kura 8 sawa na Asilimia 100 za kura zilizopigwa na Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Hadija Kibaya nae amepata kura 8 sawa na Asilimia 100 za kura zilizopigwa.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.