Februari 18, 2025 Ikiwa ni Maandalizi ya ujio wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani,Mkoani Tanga kumekuwa na maandalizi ya usafi katika Halmshauri ya Wilaya ya Muheza.
Balozi wa Mazingira nchini Tanzania Bw.Michael Msechu ameongoza usafi wa Mazingira katika Wilaya ya Muheza katika matayarisho ya kumpokea Rais Dkt Samia Suluhu katika Ziara yake itakayofanyika Tarehe 23/2/2025 Wilayani hapa.
Usafi huo umeanza kwa kusafisha barabara kuu kuanzia kituo cha mafuta cha BP mpaka mtaa wa Majengo Shimoni kwa kutumia Boza la Maji na baadae kufanya usafi maeneo ya stendi ya mabasi,Amtico,Mashine nyingi,soko la samaki na uwanja wa Mpira wa Jitegemee.
Katika Maandalizi hayo Michael Msechu amesema kuwa Dkt samia tayari ameleta Fedha kiasi cha Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya Maendeleo na ameahidi kukabidhi mapipa matano katika soko la samaki kwa ajili ya kuhifadhia taka.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah,Dkt Fani Mussa na Afisa Tarafa wa Wilaya Ally Kijazi Kwa pamoja wameshirikiana na Wananchi kufanya usafi katika mitaa mbalimbali na kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kumpokea Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.