Wanawake wa Wilaya Muheza wametoa taulo za kike zaidi ya 400 kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya za Msingi, Sekondari na chuo cha ufundi kiwanda wakati wakiadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kwa kawaida hufanyika kila mwaka Machi 8,ili kuwafanya wajiamini muda wowote wawapo kwenye hedhi.
Taulo hizo zimetolewa kwa watoto wenye mahitaji maalum waliopo katika Shule ya Msingi Masuguru ,Muheza, na Mbaramo pia wanafunzi wa Sekondari Songa pamoja na chuo cha ufundi Kiwanda nao walinufaika.
Makabidhiano ya Taulo hizo yamefanyika siku ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika jana tarehe 7/3/202 Shule ya Sekondari Songa na leo tarehe 8/3/2021 Shule ya Msingi Masuguru na Muheza.
Akizungumza katika hafla hiyo Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Muheza vije Mfaume Ndwanga amesema lengo la kutoa taulo hizo ni kuwasaidia wanafunzi hao ambao wengi wao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria vizuri shuleni hali itakayopelekea kuwa na ufaulu usioridhisha shueni humo.
Katika tukio jingine wanawake wa Wilaya Muheza walitoa msaada wa mifuko ya Saruji itakaosaidia katika ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum uliopo katika Shule ya Msingi Masuguru.
Nao wanafunzi hizo waliwashukuru sana wakina mama wa Muheza kwa Msaada huo wakisema kuwa utawafanya wajisikie huru hatimaye kupunguza idadi ya watoro shuleni.
|
|
|
|
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Erasto Jerome Mhina (mwenye suti nyeusi) akisaidia kukabidhi mifuko ya sauji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili isaidie kukamilisha bweni la wattoto hao mbalo mpaka sasa liko katika hatua ya upauaji. | Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Mhe. Erasto Jerome Mhina (mwenye suti nyeusi) akishirikiana na wanawake wa Muheza kukabidhi taulo za kike jana tarehe 8/3/2021. | Sehemu ya Wananchi na Watumishi wa Muheza walioshiriki katika zoezi la ugawaji wa taulo za kike na saruji lililotolewa jana tarehe 8/3/2021 Shule ya Msingi Masuguru. | Sehemu ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Masguru, Mbaramo na Muheza wenye mahitaji maalum walioshiriki kwenye hafla hiyo iliyofanyika tarehe 8/3/2021 katika Shule ya Msingi Masuguru. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.