Halmashauri ya wilaya Muheza imekopesha kiasi cha shilingi 116,800,000 katika kipindi cha Mwezi juni 2020 kupitia mapato yake ya ndani na marejesho ya mikopo ya awali ikiwa fedha hizi zimekopeshwa bila riba na kurejeshwa baada ya miezi 3 ili kuwakwamua kiuchumi wananchi wa Wilaya hiyo.
Akisoma taarifa ya Utoaji Mikopo afisa maendeleo ya jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga amesema pesa hizo zimekopeshwa kwa vikundi 18 ambapo vikundi vya wanawake 11 vikipatiwa kiasi cha Shilingi 55,000,000 na vikundi vya vijana 7 vikikopeshwa kiasi cha shilingi 61,800,000 ambapo pesa hizi zimenunua pikipiki, cherehani na dawa za kutengenezea sabuni.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivi imefanyika katika eneo la ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Muheza ikiongowa na Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajab Tumbo wakiwemo Watumishi na wajasiriamali waliopatiwa mikopo hiyo.
aliendelea kuwa kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 Halmashauri ya Wilaya Muheza imetenga kiasi cha Shilingi 248,000,000 kwa ajili ya vikundi 42 ambapo Shilingi 130,341,000 zimekopeshwa kwa vikundi 24 katika kipindi cha mwezi April 2020 na vikundi 18 vikipata 116,800,000 mwezi juni 2020 sawa na Shilingi 247,141,000
|
|
|
|
|
|||
|
|||
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.