Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ameongoza baraza la wafanyakazi Siku ya Alhamisi tarehe 2/4/2020 katika ukumbi wa Halmashauri na kuwataka Wafanyakazi kuzingatia nidhamu ya kazi baada ya kuona kupata taarifa kuwa watumishi kumi walifukuzwa kazi katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018
Akizungumza katika baraza hilo Mmbagga amesema wafanyakazi 10 kufukuzwa kazi sio jambo zuri katika Halmashauri hali hii inaonesha kwamba nidhamu ya kazi imeshuka miongoni mwa watumishi hivyo basi niwatake viongozi wa vyama vya wafanyakazi kulisimamia jambo hili kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wanafuata kanuni na taratibu za utumishi wa Umma zilizopo kwa Mujibu wa sheria za utumishi wa Umma.
Vile vile amewataka watumishi kufuta itifaki ya uongozi kwamba wanapopatwa na matatizo wasikimbilie kwenye Uongozi wa vyama vya wafanyakazi na ngazi nyingine za juu kabla ya kuonana na uongozi husika .
“iwapo mtumishi umepatwa na tatizo unatakiwa kumuona Mkuu wako wa Idara kwanza yeye ndio atakupa maelekezo ya ngazi ipi ya uongozi ya kufuata baada ya kukusikiliza shida zako na sio kuanzia kwenye uongozi wa chama cha wafanyakazi kama ambavyo baadhi ya walimu wanafanya” alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Kwa upande mwingine alimtaka Katibu wa baraza la Wafanyakazi ambaye ni Mtendaji wa Mamlaka ya Mji JOHARI MTANGO kwenye baraza lijalo kuwe na Agenda ya kuzungumzia jinsi ya kumsaidia mtumishi wa umma wa Muheza aishi katika maisha ya kufurahia kazi pindi awapo kazini na atakapomaliza muda wake wa kazi( amestaafu).
“nikutake katibu wa baraza hili katika kikao kijacho kuwe na agenda itakayozunumzia namna ya kumsaidia mfanyakazi utakuta Mtumishi ana miaka 6 hadi 7 kazini hana hata kiwanja na nyumbani alikotoka wala hapa anapoishi sasa na hata akiwa kiwanja hana uwezo wa kupeleka hata “trip” moja ya mchanga wala jiwe, nataka tuwe tunazungumzia hali halisi ya maisha ya mfanyakazi na kutafuta namna ya kumsaidia, mfano tunapima viwanja tunauza wafanyakazi wetu hawana viwanja” alisema Mkuregenzi Nassib.
Kwa upande wake afisa utumishi Wilaya Muheza GODHELP RINGO alitoa jibu ya swali lililoulizwa kuhusu uchelewaji wa pesa ya Mazishi kuwa inatokana na mchakato wa mfumo wa utoaji wa fedha hiyo ambao hufuata kanuni za kiserikali za utojiaji wa fedha za matumizi, na kuwataka kuwa na subira wakati wa msiba unapotokea ikiwa ni pamoja ya kumpa muda mwajiri aandae malipo hayo kwani hakuna pesa ya mazishi ambayo haitoweza kulipwa na kuendelea kuwasisitiza kutopeleka malalmiko yao ngazi za juu.
Aidha akisoma taratibu za Mtumishi wa Umma kupandishwa /kubadilishwa cheo Afisa utumishi Lazaro Lemurua amesema Masuala ya yote upandishwaji wa vyeo unazingatia kanuni za kudumu za utumishi wa Umma toleo la Mwaka 2009, miundo ya maendeleo ya Utumishi ya mwaka 2002 kwa kada husika pamoja na marekebisho na miongozo kutoka kwa katibu Mkuu, Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora.
Aliongeza kuwa zoezi la upandishwaji veo mchakato wake huanzia kwenye mwaka wa fedha husika ambapo Mwezi Desemba Wakuu wa Idara huandaa bajeti ya watumishi watakaopandishwa/kubadilishwa vyeo.
Kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 watumishi 398 walipandishwa vyeo, idara ya Elimu Msingi 199, Elimu Sekondari 137, Afya 43, utawala 9, kilimo 6 na Mifugo 4 kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imepokea Ikama ya watumishi kwa barua ya tarehe 17 january 2020 jumla ya nafasi 2,201, Ajira Mpya nafasi 193, kupandishwa vyeo watumishi nafasi 504, nafasi ya Uteuzi 3 na kubadilisha vyeo watumishi 38.
katibu msaidizi wa baraza la wafanyakazi akizungumza wakati wa baraza | watumishi wakiwa katika baraza la wafanyakazi | |
katibu msaidizi wa baraza la wafanyakazi Herieth Nyangassa (kulia) wa kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji Nassib MMBAGGA wa mwisho ni katibu wa Baraza Johari Mtango na akizungumza wakati wa baraza la wafanyakazi lililofanyika tarehe 2/4/2020 katika ukumbi wa Halmashauri. | Afisa utumishi Lazaro Lemurua akisoma taarifa ya taratibu za kupandishwa cheo au kubadilishwa cheo katika baraza hilo |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.