Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa ongezeko la asilimia 23.3 la Mshahara linalotarajiwa kuanza rasmi mnao Mwezi Julai 2022.
Akizungumza wakati wa mahojiano na vyombo vya habari yaliyofanyika mnamo siku ya jumatatu tarehe 16/5/2022, katika eneo la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Muheza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe Halima Bulembo amesema ongezeko hili litasaidia kuongeza uwajibikaji katika shughuli mbalimbali za kiserikali.
Aliongeza kuwa ni Mwaka wa sita sasa watumishi hawajaongezewa mshahara lakini kupitia Serikali sikivu awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassani jambo hili limewezekana hivyo basi tunamuombea kila la kheri rais wetu.
“Rai yangu kwenu watumishi wenzangu tufanye kazi kwa bidi bila kushurutishwa, tuzingatie maagizo ya serikali na kuyatekeleza kwa wakati ili tusimvunje moyo Rais wetu Samia Suluhu hassan, tufanye kazi kwa bidi ili aweze kuona mabadiliko katika utendaji kazi wetu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Bw. Edward Mgaya amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuleta tija katika Halmashauri hiyo.
Nae Kaimu afisa utumishi Wilaya ya Muheza Lazaro Lemurua amemshukuru Rais Samia kwa ongezeko na kusema kwamba ameupiga mwingi na kuahidi kuwataka watumishi kuzingatia maadili na nidhamu ya kazi ikiwa kama ishara ya kumuunga mkono mhe rais.
Kwa upande Swaumu Mohamedi mtunza kumbukumbu katika Halmashauri hiyo amesema ongezeko hilo la mshahara litasaidia kujenga nyumba, kununua kiwanja, kusomesha watoto na kumalizia nyumba ambazo bado hazijakamilika za watumishi.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.