Watendaji wa Kata wameombwa kusoma taarifa za Mapato na Matumizi kwa Wananchi ili kuweza kuondoa wasiwasi kwa Wananchi juu ya matumizi ya Pesa zinazotolewa kwa ajili ya Maendeleo. Akizungumza Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza Mhe. Mohamed Hassan Moyo katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 11/03/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Vilevile Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari wamesisitizwa kuhakikisha Taarifa za fedha za Elimu bure zinabandikwa kwenye mbao za matangazo ili Wananchi waweze kufahamu kazi inayofanywa na Serikali ya Dk. John Pombe Magufuli “ naomba sana taarifa za fedha za elimu bure zinazokuja kila Mwezi zibandikwe kwenye mbao za Shule ni muhimu sana Wananchi kufahamu matumizi ya fedha hizi” amesema Mhe. Diwani Makame Seif Abdalah.
Sambamba na hayo Katibu wa CCM Wilaya, Mhe. Mohamed Hassan Moyo amewaomba Madiwani kuwa na ushirikiano ili kuleta maendeleo katika Kata “naomba muwe na mahusiano mazuri mpendane ili muweze kufanya kazi kwa pamoja hata kupelekea maendeleo katika kata zenu maendeleo huja kwa kushirikiana” amesema Katibu wa CCM Wilaya Mhe. Mohamed Hassan Moyo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.