Watendaji wa kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 28/1/2022 katika ukumbi wa mikutano wa walimu (CWT) wamepatiwa mafunzo ya Anwani za Makazi ili kuwajengea uwezo jinsi ya kuweka namba za utambulisho wa makazi kwenye maeneo wanayofanyia kazi.
Akifungua mafunzo hayo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye pia ni afisa utumishi wa Wilaya hiyo GODHELP RINGO amewataka watendaji wa kata na vijiji kuzingatia mafunzo hayo ili wakirudi kwenye maeneo yao wakatoe elimu stahiki kama walivyoelekezwa na wawezeshaji.
Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za makazi MKUMBO LEVI NGOI ameelezea maana ya Anwani ya Makazi kuwa ni utambulisho wa mahali,/ mtu kitu kwenye uso wa Nchi wenye lengo la kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.
Nae Afisa Mtendaji kijiji cha Gare kilichopo katika kata ya Magoroto Wilayani Muheza Shabani Kinyasi amesema zoezi la Anwani za Makazi lina umuhimu sana katika jamii kwa kuwa litarahisisha upatikanaji wa mtu pindi unapomuhitaji, pia utarahisisha uunuzi wa bidhaa.
Aliendelea kuwa kwa kuwa zoezi hili ni jipya katika jamii, wananchi wengi hawana uelewa nalo watajitahidi kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kutoa ushirikiano wa karibu kwa watu watakaofika katika maeneo yao.
Mratibu na afisa mipango miji wakiteta | sehemu ya wawezeshaji | sehemu ya watendaji walioshiriki | watendaji waliochangia mada |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Mratibu wa Anwani za Makazi Mkumbo Levi Ngoi (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na afisa mipango miji wa wilaya muheza Thomas Mkwavi wakati wa mafunzo hayo yakiyofanyika katika ukumbi wa CWT leo tarehe 28/1/2022. | Sehemu ya wawezeshaji waliotoa mafunzo kwa watendaji | sehemu ya watendaji wa kata na vijiji waliohudhuria mafunzo hayo | Sehemu ya Watendaji wa kata na vijiji waliochangia mada wakati wa mafunzo |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.