Msimamizi wa Uchaguzi Mkoa wa Tanga (kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi) Bi Phina Benard amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata ambao ni watendaji kata kuhakikisha wanachukua tahadhali ya ugonjwa wa Corona wakati wa Zoezi la Uandikishaji kwa kuhakikisha wananchi wote wanaofika katika vituo vya uandikishaji wanawe maji na sabuni.
Akizungumza katika Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura awamu ya Pili yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tate plus tarehe 15/4/2020 ambapo watu 130 walishiriki Msimamizi wa Uchaguzi Mkoa wa Tanga amesema lengo la kuchukua tahadhali ni kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona .
“Tumehakikisha kila kituo kinakuwa na vifaa vya kujikinga na maambukizi ya corona, kama vile ndoo za maji kwa ajili ya kunawa mikono, vitakasa mikono( sanitizer) “ spirit kwa ajili ya kusafisha mashine, barakoa, “gloves” na vifaa vingine, nawaagiza watendaji wa kata kusimamia kila mwananchi anayefika kujiandikisha anafuata taratibu za kiafya ili kuweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu” alisema PHINA.
Akitoa maelekezo ya unawaji na uvaaji wa gloves Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza Rehema Akida amesema kwamba unapovua gloves hutakiwi kuirudia tena na unatakiwa uihifadhi vizuri namna ambayo mtu mwingine hawezi kuishika, na hakikisha unanawa mikono au unapaka kitakasa mikono kila unapomuhudumia mwananchi , epuka kumgusa mtu yoyote unapomhudumia.
Kwa upande wake Afisa Tehama wa Halmashauri ya Wilaya Muheza EMMANUEL MARO amewataka waandikishaji na BVR OPERATORS wanapitia taarifa za mpiga kura kwanza ndipo wamsajili ili kuepuka makosa madogo madogo, pia amewataka kuzingatia muda wa kufungua kituo saa 2:00 asubuhi na kufunga saa 12:00 jioni.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.