Mwakilishi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza ambaye ni Afisa Uchaguzi Wilaya Muheza NMtakwimu wa Wilaya hiyo Nelson Mwankina jana tarehe 24/10/2020 amefunga mafunzo ya siku mbili yaliyoanza tarehe 23/10/2020 na kukamilika siku hiyo kwa kuwataka wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo kuzingatia elimu walioipata wakati wa mafunzo.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Mwankina amewataka wasimamizi hao kutokuwa na mashabiki wa vyama vya siasa kufanya hivyo kutapelekea uvunjifu wa Amani kwenye vituo vya kupigia kura .
Aliongeza kuwa siku ya Uchaguzi tarehe 28/10/2020 , mtu yeyote haruhusiwi kuvaa vazi au sre inayoashiria chama chochote kile na atakaefanya hivyo kabla hajaingia kwenye kituo cha kupigia kura Mlinzi wa Kituo atawajibika kumtoa kituoni mtu huyo.
Akiendelea kutoa ufafanuzi wa sifa 3 za mtu atakaeruhusiwa kupiga kura,amesema antakiwa kuja na kadi ya mpiga kura na msimamizi wa ucghaguzi ahakikishe jina la mtu huyu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lililopo kituoni kma yumo,
Ikiwa sifa ya pili ni kwa mpiga kura ambaye atakuwa amepoteza kadi yake, siku ya kupigia kura atatakiwa kwenda kituoni akiwa na kitambulisho cha uraia, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria nje ya Nchi ikiwa majina yaliyopo kwenye kitambulisho chake yatafanana na yale yaliyopo kwenye daftari la mpiga kura.
Katika hatua Nyingine Mtu anayetakiwa kupiga kura ni Yule ambaye hana kitambulisho cha mpiga kura, picha iliyopo kwenye daftari haionekani vizuri lakini majina yanafanana na hayo atakayomtajia Msimamizi msaidizi wa kituo namba moja.
Sambamba na hayo aliendelea kuwasisitiza wasimamizi wa vituo kuwahi mapema siku ya kupiga kura kabla ya saa 12:00 asubuhi ili waweze kuondoa mabango machapisho, yaliyowekwa na wagombea kipindi cha kampeni pamoja na kuweka mpangilio mzuri wa kituo cha kupigia kura ili ifikapo saa 1:00 asubuhi zoezi la upigaji kura lianze.
Katika hatua nyingine amewataka wasimamizi hao kuwa makini wakati wa makabidhiano ya vifaa kwa kuhakikisha wanpewa vifaa vitakavyotosheleza vituo watavyokwenda kuvifanyia kazi, kushindwa kufanya hivyo kutaleta usumbufu na kupelekea zoezi lisiwe na ufanisi . pia jukumu la ulinzi wa vituo hivyo ni la kwao.
“Msimamizi ukishakabidhiwa vifaa kwa maandishi ni vya kwako , umekwenda navyo nyumbani, umelala navyo kitandani, umepeleka kituoni sisi haituhusu na iwapo vitapotea utawajibika kwa namna moja au nyingine “ alisema Nelson.
Aidha amewataka wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha wanaweka kituturi mahali ambapo kuna usiri ili kumfanya mpiga kura kuwa huru kumpigia kura mgombea anaemtaka.
Kwa upande Mwingine amewataka wasimamizi wa Vituo kuwasilisha Matokeo ya Uchaguzi haraka iwezekavyo kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata mara baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu matokeo na kubandika matokeo vituoni.
|
|
|
|
|
|
||
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.