Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo amewataka wanawake kuchangamkia fursa za kiuchumi na kielimu ili waweze kufikia malengo na ndoto walizonazo katika maisha yao. Ameyasema hayo alipokuwa Mgeni rasmi wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani kilichofanyika Marchi 8, 2022 katika Shule ya Msingi Lusanga na kuhudhuriwa wanawake wa Asasi za kiserikali, Binafsi, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza, Madiwani wanawake, Mbunge wa jimbo la Muheza Mhe. Hamisi Mwinjuma almaarufu MWANA FA, na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lusanga.
Akizungumza katika sherehe hizo Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wanawake kujiendeleza kielimu wasiishie na kuridhika na Elimu walizonazo ili waweze kuwa na mafanikio mazuri katika maisha yao pasipokuwategemea wanaume zao.
Pia amewataka wakina mama kuwa na malezi bora kwa watoto wao kwa kuwatia moyo pale inapotokea wamekosea na kufeli katika harakati za kielimu ili kuwaepusha na maamuzi magumu wanayoweza kuchukua baada ya kuona wameshindwa na kubezwa na jamii inayowazunguka.
Vile vile amewataka kuanzisha miradi midogo midogo kukwepa kuwa ombaomba kwa kwa waume zao.
“Wakina mama wenzangu tusibweteke kwa kukaa majumbani bila shughuli yeyote tujitahidi japo tufungue miradi midogo midogo ya kuweza kutusaidia katika matumizi ya nyumbani sio kila kitu utegemee kuomba kwa mume wako atakuchoka na kukudharau, baba akilipia maji wewe lipia umeme” alisema Mhe Bulembo.
Aliendelea kutoa rai kwa wanawake wenye tabia ya kunyanyasa watoto wa waume zao na ndugu wa karibu kwa kuwachotesha maji na kuwapangia wakati wa kujisomea kuacha tabia hiyo mara moja kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Muheza kupitia Chama cha Mapinduzi Hamisi Mwinjuma amesema wanawake ni jeshi kubwa ambalo wanaweza kufanya maamuzi katika jamii hivyo basi waendelee kujiendeleza ili waweze kuwa viongozi wakubwa kama ilivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wanawake waliopo katika nchi hii.
Awali akitoa historia ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Muheza Bi. Vije Mfaume Ndwanga amesema Siku ya wanawake duniani hufanyika duniani kote kila Mwaka mnamo mwezi Machi 8 ikiwa lengo ni kuweka bayana masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake kama vile ukatili wa kijinsia unaofanyika kwenye kundi hili lenye uhitaji maalum.
Wanawake wakiwa kwenye maandamano kutoka Bomani hadi Shule ya Msingi Lusanga |
|
Maandamano ya wanawake yakiwasili katika Shule ya Msingi Lusanga | Mbunge Hamisi Mwinjuma akiungana na wanawake katika kucheza Muziki wa asili ya kibondei | Mgeni rasmi akikagua mabanda ya wanawake wajasiriamali |
|
||||
|
||||
|
||||
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.