Wananchi watakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Makarani wa Sensa wanaofika katika kaya zao ili waweze kufanya kazi yao kwa weledi na ufanisi mkubwa katika muda uliopangwa na kutimiza adhima ya Serikali ya kumtaka kila Mwananchi ahesabiwe kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 24/8/2022 ofisini kwake, Mratibu wa Sensa Wilaya ya Muheza ambaye pia ni afisa takwimu wa Wilaya hiyo Ndugu Nelson Mwankina amesema Zoezi hilo la Sensa litafanyikawananchi wahakikishe wanaandaa mapema taarifa za wanakaya waliolala katika kaya yake usiku wa kuamkia siku ya sense yaani tarehe 23/8/2022.
Aliongeza kuwa Mkuu wa kaya ahakikishe anakuwa na vitambulisho vya vya NIDA, Kitambulisho cha mpiga kura, Bima, ya afya na taarifa sahihi za wanakaya wake ili kurahisisha na kupunguza muda wa karani kukaa katika kaya yake kwa muda mrefu nakumsaidia karani akahudumie wanakaya wengine.
“Nitoe wito kwa wananchi wa muheza pale karani anapotaka taarifa atoe kwa wakati, chonde chonde wananchi wa Muheza tunaomba ushirikiano wenu ili zoezi hili lifanikiwe kwa asilimia kubwa” alisema Mwankina.
Nae Amina Hatibu Ally kijana wa Miaka 24 mkazi wa Ubena kata ya Tanganyika ambaye amehesabiwa jana tarehe 24/8/2022 ametoa wito kwa vijana wenzake kujitokeza kuhesabiwa ili kuisaidia Serikali kupanga Mipango ya maendeleo ya Vijana.
“nawasihi vujana wenzangu wajitokezekwa wingi kuhesabiwa kwa kuwa Rais wetu akiona vijana wengi wamejitokeza kuhesabiwa na hawana ajira atatusaidia kupata ajira kwa maendeleo ya taifa letu” alisema Amina.
|
|
|
Karani wa Sensa (kushoto) akifanya mahojiano na Maimuna Ally mkazi wa Ubena kata ya Tanganyika Muheza jana tarehe 24/8/2022 | Maimuna Ally akizungumza mara baada ya mahojiano na karani wa sensa | Amina Hatibu miongoni mwa watoto wa Maimuna Ally aliyelala katika kaya hiyo usiku wa tarehe 23/8/2022 akizungumza mara baada ya mahojiano na karani wa sensa |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.