Wananchi wametakiwa kumuenzi aliyekuwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Wiliam Mkapa kwa kuzingatia mambo aliyoyafanya kipindi cha uhai wake yakiwemo Masuala ya Uwazi na Ukweli.
Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa Ibada Maalum ya Maombolezo iliyofanyika jana tarehe 28/7/2020 Wilayani Muheza katika Viwanja vya Jitegemee iliyoongozwa na Mkuu huyo wa Wilaya na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, Taasisi mbalimali, watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na Wananchi wote.
Mhe, Mkuu wa Wilaya amesema wananchi wa Wilaya hiyo walikuwa wakimuona hayati Mkapa akipita Wilayani humo akitokea uwanja wa ndege Jijini Tanga akielekea Lushoto na kwa sasa hawawezi kumuona tena hivyo waendelee kumuenzi na kumuombea.
“Ndugu zangu wana Muheza tulikuwa tunamuona Hayati Mkapa akipita hapa kwetu akitokea Uwanja wa ndege Tanga na kuelekea Wilayani Lushoto na sasa hatutamuona tena hivyo tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amina” alisema Mwanasha.
“Rais Mkapa alitupikia Uji akaweka bluu bendi, na Sukari akatunywesha hivyo tumuombee kwa mola wetu amlaze mahali pema peponi Amina” alisema Mkuu wa Wilaya.
Alisema kwamba Msiba huo ni wa watu wote na Rais Magufuli, mke, watoto, na wajukuu wa Marehemu wako katika wakati Mgumu hivyo tuendeleze maombi ambayo yatakuwa faraja kwao.
Vile vile alisema kwamba wao kama Wilaya wanatoa Salamu za Pole kwa familia, ndugu, Jamaa na marafiki na kuwaombea kwa Mola azidi kuwapa faraja katika kipindi hiki kigumu.
Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Muheza Laicky Gugu amesema Mkapa ni Kiongozi Mpiganaji aliepelekea kuanzishwa kwa Mfuko wa jamii wa TASAF, Pia alianzisha MEMKWA( ambapo lengo la Memkwa ni kutoa elimu kwa walioikosa )
Aliongeza kuwa Mkapa alikuwa Mshauri Mzuri ndani ya Chama cha Mapinduzi na hivi karibuni kabla ya kura za maoni alikuwa miongoni Mwa Wanachama waliokuwepo Dodoma ambako alitoa ushauri na mara nyiki amekuwa akijenga hoja na kuzitetea.
Nao wasanii wa Muziki Tanzania Hamisi Mwinjumaalimaarufu Mwana FA, na Mwana muziki nguli Nguza Viking alimaarufu Babu Seya wamesema kifo cha aliyekuwa rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kimewaumiza na ni pigo sana kwao kwa kuwa yeye ndie Mwanzilishi wa COSATA ambaya ni taasisi ya kusimamia haki miliki za wasanii.
MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE, MWANASHA TUMBO AKIZUNGUMZA WAKATI WA IBADA. | KATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUANZA KWA TUKIO LA IBADA | VIONGOZI WA VYAMA VYA KISIASA WAKIZUNGUMZA MARA BAADA YA IBADA MAALUM YA MAOMBOLEZO | SEHEMU YA WANANCHI WAKIWA KATIKA ENEO LA MAOMBOLEZO | VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA HAFLA YA MAOMBOLEZO ILIYOFANYIKA UWANJANI JITEGEMEE. | WANANCHI WAKIWA KWENYE FOLENI YA KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO | VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA MUHEZA WAKIWA KATIKA IBADA MAALUM YA MAOMBOLEZO YA RAIS MSTAAFU HAYATI BENJAMINI WILIAMU MKAPA UWANJANI JITEGEMEE. | MWANAMUZIKI NGULI NGUZA VIKING ( MWENYE FLANA NYESI) AKIWA NA MKE WAKE AMBAYE NI KATIBU TAWALA WILAYA YA MUHEZA BI DESDERIA HAULE PAMOJA NA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA TANGA NA WA MWISHO NI MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA HAMISI MWINJUMA MWANA FA AKIZUNGUMZA BAADA YA IBADA. |
|
WATU MBALIMBALI WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO |
|
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
|
|
|
|
|
|
|||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.