Wananchi wametakiwa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (ICHF) ambao ni mpango wa uchangiaji wa hiari wa huduma za afya kabla ya kuugua ili kuiwezesha familia kutibiwa kwa gharama ya shilingi elfu 30 kwa mwaka mmoja.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (ICHF) uliofanyika katika kijiji cha Kweisaka(Bombani) tarehe 25/6/2021 kata ya Tongwe Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Abdalla Bulembo amewataka wananchi kukata Bima kabla ya kuugua ili wapatapo maradhi waweze kutibiwa bila kuchangia pesa nyingine.
“Kipaumbele cha Serikali awamu ya sita (6) inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kutatua changamoto za afya, kuhakikisha uwepo wa dawa, uwepo wa wataalam, vitendea kazi na vitendanishi hivyo basi tukate bima mapema kwani ugonjwa haupigi hodi” alisema Mkuu wa Wilaya Muheza.
Aliendelea kuwa iwapo kaya ya watu 6 au chini ya idadi hiyo watajiunga katika mfuko huo wana uwezo wa kutibiwa katika Zahanati, kiyuo cha Afya, Hospitali ya Wilaya na Hospitali ya Mkoa kwa rufaa maalum kutoka katika kituo husika
Aidha amewataka wananchi kufuga mifugo, kama kuku, mbuzi, kondoo, bata na ngombe wakiuza ziwasaidie kujiunga kwenye Bima ya Afya iliyoboreshwa( ICHF) kwa kuwa ugonjwa haupigi hodi mtu anaweza akaugua halafu akawa hana pesa ya kwenda Hospitali.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Erasto Jerome Mhina ametoa mchango wa shilingi laki moja kwa kaya 5 zilizo tayari zichangia kiasi kilichobakia cha shilingi elfu 10 ili wapatiwe kadi za CHf iliyoboreshwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za jamii na kujitegeme ambaye pia ni diwani kata ya Genge Mhe Mosses Kisiki amewataka vijana wa boda boda kuhifadhi kiasi cha shilingi mia tano (500) kila siku ambapo ndani ya siku 60 itawasaidia kupata fedha kiasi cha shilingi 30,000 kitakachowawezesha kujiunga kwenye mfuko wa ICHF.
“ Afya ni mtaji ndio maana wote tuko hapa leo, mfuko huo ni mali yetu, ni kapu linaloratibu huduma za afya hivyo tuungalie kwa jicho pana ewe, baba mama, kijana jiunge kwenye mfuko huu mapema ili uweze kutibiwa bila usumbufu” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Bw. JOHN BONIFACE MNGOMA.
Awali akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mratibu wa mfuko wa Afya ya jamii wilaya Muheza Hadija Chanyendo amesema Mfuko wa Afya ya jamii ulioboreshwa unatekelezwa kwa sharia NO. 1 ya mwaka 2001 ambapo wilaya ya Muheza imeanza kutekeleza mpango huu tangu Mwaka 2019.
Aliendelea kuwa mpango wa kumsajili Mwanachama wa Bima hufanyika kwenye ofisi ya Mtendaji wa kijiji kwa kutumia teknolojia ya simu ambayo imemuondolea gharama ya kupiga picha mwanachama pamoja na usumbufu wa kuifuata huduma mbali na anapoishi.
Akitaja kiwango cha kulipia Mratibu huyo wa CHF amesema ni shilingi elfu thelethini (30,0000) kwa Mwaka Mzima kwa kaya yenye watu wasiozidi sita(6) yaani baba, mama na watoto(wategemezi) wenye umri chini ya miaka 18.
Aliongeza kuwa lengo ni kusajili kaya 47,920 ifikapo juni 2021 mpaka sasa jumla ya kaya 1273 zimejiunga ikiwa ni sawa na asilimia 2.6 hivyo basi wananchi wajiunge kwa wingi ili kuongeza huduma ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya.
DC MUHEZA AKIZUNGUMZA | KAIMU DED AKIZUNGUMZA | DMO AKIZUNGUMZA | DC AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA | MRATIBU CHF AKISOMA RISALA | MWENYEKITI BODI YA AFYA AKIZUNGUMZA |
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa uliofanyika katika kijiji cha Kweisaka kata ya Tongwe tarehe 25/6/2021. | Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo Bi. Happiness Laizer akizungumza wakati wa uzinduzi. | Mganga Mkuu Wilaya ya Muheza Bi. Flora Kessy akizungumza katika uzinduzi huo. | Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Muheza mara baada ya Uzinduzi wa CHF iliyoboreshwa uliofanyika katika kijiji cha Kweisaka/ Bombani kata ya Tongwe tarehe 25/6/2021. | Mratibu Mfuko wa Afya ya jamii Wilaya ya Muheza Bi. HADIJA CHANYENDO(kushoto) akisoma risala kwa mgeni rasmi juu ya uzinduzi wa CHF iliyoboreshwa | Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Wilaya ya Muheza Bw. JOHN BONIFACE MNGOMA akizungumza wakati wa uzinduzi tarehe 25/6/2021 katika kijiji cha Kweisaka /Bombani kata ya Tongwe. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.