Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Dk. Flora Kessy amewataka Wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ICHF. Ili kuweza kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea Huduma Wilayani Humo. Akizungumza katika zoezi la upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza katika uwanja wa Jitegemee 22/2/2020 Amewaeleza Wananchi umuhimu wa kujiunga na ICHF unasaidia kuwepo kwa dawa za kutosha katika vituo vya afya ameeleza Pesa zinazopatikana katika ICHF hutumika kuongezea kununua dawa.
Vilevile mganga Mkuu amewataka Wananchi kufanya mazoezi ya viungo vya mwili ili kuweza kujikinga na Magonjwa yasiyoambukiza kama vie kisukari, shinikizo la damu, Magonjwa ya Moyo, pamoja na Magonjwa sugu yasababishayo kuziba kwa mfumo wa upumuaji “mazoezi yanajenga mwili, kulinda mwili, na kukinga mwili na maradhi” amesema Mganga Mkuu Dk. Flora Kessy.
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwanasha Rajab Tumbo alipata nafasi ya kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kufanya mazoezi, kupima magonjwa yasiyoambukiza na kuchangia Damu kwaajili ya kuokoa maisha ya Watu. Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha Wananchi wanapata Huduma za Afya nzuri “ tunategemea kuanza kutoa huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza hivi karibuni” amesema Mwanasha Tumbo Mkuu wa Wilaya Muheza.
Aidha zoezi la huduma Mkoba lilianza tarehe 05/02/2020 na kuitimishwa Jumamosi leo tarehe 22/02/2020 katika tarafa ya Muheza kwa kupima Sukari, Shinikizo la Damu, uwiano wa urefu na uzito, uchunguzi wa macho na uchangiaji wa damu kwa hiari. Jumla ya Kata 12 Wilayani Muheza zilifikiwa na kupata huduma “tumeweza kuwafikia na kuwapa huduma jumla ya Watu 1416, Wanawake 866 na Wanaume 550” amesema Dr Elius Bahindi alipokuwa akisoma Taarifa fupi.
Mhe. Mwanasha Rajab Tumbo akipima afya katika zoezi la kupima Magonjwa yasiyoambukiza katika Uwanja wa jitegemee leo tarehe 22/02/2020 | Mkuu wa Wilaya (katikati) pamoja na Wananchi wa Muheza wakifanya mazoezi ya Viungo vya Mwili | Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwanasha Tumbo akiongea na Wananchi katika uwanja wa Jitegemee baada ya kutoka kufanya mazoezi ya Mwili |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.