Wakulima wa Mazao ya Viungo Wilayani Muheza Mkoani Tanga Wameiyomba Serikali kuviwezesha Vyama vya Ushirika (Amcos) kwani Viimekuwa vikishindwa kununua Mazao yao jambo ambalo linachangia kuuza kwa Walanguzi.
Wakulima wametoa ombi hilo kwenye Kikao cha Jukwaa la Wadau wa Mazao ya Viungo kilichofanyika Wilayani humo tarehe Desemba 1 , 2021 katika Ukumbi wa Tate Plus na kuhudhuriwa na maafisa ugani, watendaji wa kata, watendaji vijiji, maafisa tarafa, wa maeneo yanayolima mazao ya viungo.
"Kipato cha mkulima kinatokana na kuuza Mazao kwasasa vyama vya ushirika vimekuwa havina fedha ya kumlipa Mkulima pindi anapouza Mazao hivyo niwazi kuwa Mkulima anakwenda kuuza kwa Walanguzi ili aweze kupata fedha kwa ajili ya maisha yake na hata kufanya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo" Wamesema Wakulima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Mazao ya Viungo Wilayani humo Ayubu Mhina amekiri kuwepo kwa Changamoto za kifedha zinazo zikabili Amcos hizo ambapo amesema wataendelea kusimamia Maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha Wakulima wanauza mazao yao kupitia vyama hivyo lengo likiwa ni kumsaidia Mkulima kuuza kwa bei nzuri ili aweze kukuza Uchumi wake kupitia zao la viungo kwa kuweka utaratibu kuwa Wafanyabiashara wote wanapo taka kununua viungo hivyo lazima wafuate sheria ikiwemo kupitia kwenye vyama vya ushirika na sio kwenda kwa Wakulima moja kwa moja jambo amblo litasaidia hata Halmashauri kupata mapato yake.
Aidha Mgeni rasmi kwenye Kikao hicho Issa Msumari amewataka Wakulima kuendelea kuaminiana na kuongeza ushirikiano kwenye vyama vya Ushirika jambo ambalo litaweza kuwasaidia kuinua uchumi wao kwa mfumo wa kuuza kwenye vyama kuliko kuuza kwa Wafanyabiashara wanao kuja wakati wa msimu.
"kama wakulima wakiaminiana na kuwa na umoja wanapopeleka kuuza mazao yao kwenyeAmcos itasaidi mkulima kuona tija ya kilimo hicho kwakuwa yanahifadhiwa hadi pale bei itakapo kuwa nzuri " Alisema Msumari.
|
|
|
|
|
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
|
![]() |
![]() |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe, (Kulia ) Erasto Mhina akikabidhi vyeti vya kutambua Mchango wa Wadau wa Jukwaa la Viungo. | Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe, Erasto Mhina akizungumza na Wadau wa Viungo namna ya kuboresha zao hilo. | Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muheza Issa Msumari akielezea namna Wadau wanavyoweza kunufaika na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili katika kuinua zao hilo. | Kaimu Afisa Kilimo wa Wilaya ya Muheza Adamu Nyeza alipokuwa akitoa ufafanuzi namna Serikali ilivyodhamili kuwasaidia Wakulima katika kupambana na Magomjwa ikiwemo Mnyauko ambao ulilikumba zao hilo hivi karibuni | Miongoni mwa Wakulima wa Mazoa ya Viungo alipokuwa akiwasilisha Changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba Wakulima wa Mazoa hayo ikiwemo Swala ya Vyama vya Ushirika na Kuomba Serikali kuendelea kuwasaidia kupatikana kwa dawa za kukabiliana na Magonjwa mbalimbali. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.