Wadau wa Elimu wilayani Muheza wamekutana leo Tarehe 6\4\2019 katika ukumbi wa TARECU kujadili changamoto zinazosababisha kushuka kwa ufaulu wa Wanafunzi darsani ili kupata ufumbuzi wa kuwainua watoto kielimu.
Akisoma taarifa ya hali ya elimu wilayani humo Afisa Elimu Sekondari Julitha Akko amesema kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kunasababishwa na mamo mengi yakiwemo utoro wa kudumu na wa rejareja, Mimba, ubakaji, utumikishwaji, kutokuwapo kwa chakula cha mchana shuleni, Upungufu mkubwa wa miundombinu mbalimbali kama vyoo, vyumba vya madarasa maabara, Mwamko duni wa wanajamii kuhusiana na elimu , unyanyasaji wa kijinsia , Mila na desturipotofu pamoja na madawa ya kulevya . kwa mwaka 2017\2018 idadi ya mimba imeongezeka sana hasa kwa Shule za Sekondari kutoka wanafunzi 24 mwaka 2017 hadi 35 mwaka 2018.
Aliongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya Muheza imeanzisha na kuendeleza wa mradi wa ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Msingi Mbaramo , hadi sasa ujenzi jengo moja limefikia hatua ya kupandisha kuta na jengo la pili liko katika hatua ya kuchimba msingi. Ujenzi huu wa mabweni yote mawili unakadiriwa kutumia kiasi cha Tshs 247,997,918/
Afisa Elimu aliendelea kuwa Halmashauri ya Wilaya Muheza imeanza ujenzi wa bwalo la chakula kwa Shule ya Sekondari Songa baada ya kupokea kiasi cha Tshs 102,000,000/= ikiwemo Tshs 100,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa bwalo na Tshs 2,000,000/= kwa ajili ya ufuatiliaji, ujenzi unaendelea kwa kushirikisha nguvukazi za jamii ya Tarafa ya Bwembwera unatarajiwa kukamilika kwa muda uliopangwa .
Akiendelea kusoma Taarifa hiyo Akko amesema Serikali imetoa Tshs 225,000,000/= kwa ajili ya umaliziaji wa maboma ya madarasa 18 kwa Shule 9 za Sekondari kila moja Tshs 25,000,000/= Shule hizo ni Kwemkabala, Mkurumuzi , Shebomeza, Songa, Misalai, Kicheba, Kwafungo, ,Kilulu Kigombe, aidha fedha hizi zimetolewa na maelekezo ya kukamilisha maboma na sio kuanza ujenzi . Serikali imeelekeza ujenzi kukamilika ifikapo tarehe 25/4/2019 iwapo maoma hayatakuwepo fedha hizo zitahamishiwa Shule nyingine au Wilaya nyingine.
Nae Afisa Elimu Msingi Bi Pilli maximillan alisoma taarifa ya utekelezaji wa Kampeni yenye kaulimbiu “Ulinzi na Elimu kwa Mtoto wa Muheza ni wajibu wangu”ambayo ilizinduliwa na Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru tarehe 11/10/2018 Aidha kampeni hii ni matokeo ya ya kikao cha wadau wa elimu cha mwaka 2018.
Akizitaja shughuli zilizofanyika na utekelezaji wake maximillan amesema wameweza kuboresha na kuendweleza klab mbalimbali shuleni zinazozungumzia Afya , rika, Afya, ya uzazi , sheria , mimba za utotoni , ukatili wa motto .mfano Fema kwa Shule za Sekondari na Girl guide kwa Shul za Msingi 12 na Sekondari 25.
Kwa upande wa Wadau wa Elimu walitoa ufumbuzi wa changamoto zinzowakabili wanafunzi kuwa ni upatikanaji wa chakula cha mchana Shuleni, kuzichukulia hatua za kisheria familia zitakazo zote mbili zilizosababisha upatikanaji wa mimba kwa mwanafunzi, kukomesha ajira za utotoni, kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya, kupiga marufuku vigodoro, wadhibiti ubora watimize wajibu wao, kamati ya harambee itembelee kwenye kata na vijiji kwa kuanzia kwenye kata yenye matokeo mabovu.
Baraza la kata na watendaji wa kata wawabane wazazi kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni.
Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi mtendaji waunde sheria ndogo ya chakula shuleni Elimu itolewe kwa jamii kuhusiana viashiria vya ubakajiMfano motto akibakwa asisafishwe kwani itafuta ushahidi.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.