Vyumba vya Madarasa 67 vyenye dhamani ya shilingi Bilioni 1.42 katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza vimekamilika kwa asilimia mia na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe, Halima Abdallah Bulembo, kati ya vyumba hivyo 57 ni vya sekondari Madarasa 10 ni vya Shule za msingi.
Hafla hiyo fupi ya Makabidhiano ya vyumba vya Madarasa ilifanyika siku ya jumatano tarehe 05 januari mwaka huu katika eneo la shule ya sekondari Chifu Mang’enya ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa siasa na serikali pamoja na Wakuu wa idara wa Halmashauri
Mkuu wa Wilaya Mhw, Halima Bulembo amesisitiza kuwa ujenzi huo wa Madarasa fedha zake zilitolewa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan zitumike kujenga vyumba vya madarasa Tanzania nzima ili kuwasaidia Wanafunzi ambao wamechanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kusoma katika mazingira mazuri
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muheza Ndg, Nassib Mmbagga amesema kuwa ujenzi huo wa vyumba 67 vya madarasa ni historia ndani ya wilaya kwani haijawahi kutokea ndani ya mwezi mmoja na nusu kujengwa vyumba vingi vya madarasa kiasi hicho,ambapo ujenzi huo ungeweza kutumia miaka 21 akifafanua kuwa ujenzi huo umemaliza kabisa changamoto za upunguzu wa madarasa Wilayani humo.
“Alisema kama si ujenzi wa vyumba hivyo 67 basi wanafunzi wapatao 1440 wangekosa vyumba vya kusomea lakini kutokana na ujenzi huo changamoto hiyo imebaki kuwa historia ndani ya wilaya kwani madarasa yote yatatosheleza mahitaji ya wanafunzi.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza Erasto Mhina amekili kuwa licha ya Wananchi wa Muheza kuboreshewa maisha yao kwakupata huduma mbalimbali ikiwemo za Elimu na Afya bado fedha hizo zimeinua Uchumi wa Wananchi katika kipindi Miradi inatekelezwa zaidi ya Mafundi 773 walishiriki.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza Simon Leng’ese amewataka viongozi kwenda kuwaeleza Wananchi juu ya kazi zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania katika kuhakikisha Wanafunzi wanapata elimu na Watanzania wanapata Huduma bora ya elimu.
|
|
|
|
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Ndg, Nassib Mmbagga akimkabidhi ufunguo wa madarasa mkuu wa wilaya ya Muheza Mhe, Halima Bulembo katika hafla ya ukabidhi wa madarasa | Mkuu wa Halmshauri ya wilaya ya Muheza Mhe, Halima Bulembo akizungumza wakati wa hafla ya ukabidhi wa madarasa. | Picha za pamoja kati ya mkuu wa wilaya na watumishi mbalimbali wa serikali | Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Ndg, Nassib Mmbagga (Juu), Pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mhe, Erasto Mhina (Chini) wakizungumza kwenye hafla ya ukabidhi wa madarasa. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.