Kamati ya afya katika kuendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mh.Halima Bulembo wamepitisha mikakati mbalimbali yakukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 ikiwa ni kuwaomba viongozi wa dini kutumia nafasi zao katika kuihamasisha jamii kujitokeza katika kupata chanjo.
Hayo yamesemwa katika kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mipango wa jamii shirikishi na harakishi wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Akizungumza katika kikao hicho Mh. Bulembo amewaomba zaidi viongozi wa dini kuendelea kutumia nafasi zao katika kushauri na kuihamasisha jamii waweze kupata chanjo.
Aliongeza kuwa isiwe tu kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya kupata chanjo ya UVIKO 19, bali amewataka wataalam kutoa elimu kufuatia chanjo nyingine pia zaidi kuangalia uhifadhi wake, ili kuwezesha wananchi kupata kinga safi na salama.
Awali mganga mkuu wa Halmashauri wa wilaya ya Muheza Dr. Flora Kessy amewataka wananchi kuendelee kuchukuwa tahadhari na kuzifwata sheria zote ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu ikiwemo kupata chanjo ya CORONA, hivyo ameongeza kwamba jukumu la serikali ni kuona wananchi wake wanapatiwa chanjo kwani Taifa lenye maendeleo lazima liwe na afya.
Aidha alisema serikali imetoa kiasi cha Tsh mil 57,566.41 ili kuwezesha na kuharakisha shughuli zote pamoja na zoezi zima la utoaji chanjo katika Halmashauri yawilaya ya Muheza.
Baadhi ya viongozi walioshiriki katika hafla hiyo, ikiwemo viongozi mbalimbali wa dini, wameomba wataalam kuendelea kuielimisha jamii, ili kuweza kuwaondolea dhana potofu zilizojengeka dhidi ya UVIKO 19 na kuwaondolea hofu na zaidi wataendelea kushirikiana na wataalam wa afya kwa kutumia nafasi zao katika kuhamasisha na kushauri waumini wao waweze kupata chanjo kwaajili ya usalama wa afya zao.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mh.Halima Bulembo akizungumza na wajumbe jana katika kikao cha kujadili na kuweka mikakakti na utekelezaji wa mipamgo wa jamii shirikishi na harakishi wa chanjo dhidi ya UVIKO 19. | Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Dr Flora Kessy akielezea malengo ya kikao hicho ikiwemo na mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19. | Mwenyekiti wa kamati za huduma za jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Moses Kisiki ambaye pia ni Diwani wa kata ya Genge akitoa mchango wake jinsi yakukabiliana na UVIKO 19 katika kikao. | Baadhi ya viongozi wa dini wakichangia mawazo mbalimbali ikiwemo kukubali kutumia nafasi zao katika kuihamasisha jamii. | Mkuu wa Wilaya ya Muheza watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu, viongozi wa dini pamoja na viongozi kutoka Halmashauri. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.