Taasisis isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama (VITAL INTRUSIVE ORGANIZATION ) iliyopo jijini Tanga yenye jukumu la kuwafichua na kuwawezesha kielimu watoto wenye mahitaji maalum limewachukua watoto 3 wenye ulemavu wa macho jana kwa lengo la kuwasomesha baada ya kuona wanaishi katika mazingira hatarishi hali iliyopelekea kuacha shule.
Akitoa taatrifa ya watoto hao Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu tumbo amaliwataja watoto hao kuwa ni Samwel Chali (12), Mariki Bakari (11) na Jumaa Bakari (9) ambao walishindwa kuendelea na masomo kwasababu ya wazazi wao kushindwa kuwalipia mahitaji ya shulei kwa kuwa walikuwa na hali ngumu ya maisha.
Aidha, aalitoa wito kwa wadau wengine kusaidia kuunga mkono kuchangia ujenzib wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum kupitia tigopesa au M- pesa kwa namba ya Kampuni au Biashara 395533kwa kumbukumbu na 123 na hatimaye aliitaja kauli mbiu kuwa “Ustawi wao wajibu wetu “ alisema Tumbo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.