Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Issa Suleiman Msumari amewataka vijana kuwa na utayari na kupenda kazi zao wanazozifanya kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia wao kuwa na nidhamu na kazi zao ikiwemo kujali muda, biashara na mazingira ya kazi zao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na Kanisa Huru la Pentekoste nchini (FPCT). Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ambasador uliopo wilayani Muheza Jumamosi ya Tarehe 18, February 2023.
Ameendelea kuwaasa wajasiriamali hao kuachana na Imani potofu za ushirikina kuamini kwamba kwenda kwa mganga kutaikuza biashara kwani hiyo ni miongoni mwa dalili zinazoonyesha kuwa uwezo wa mtu kufikiri kufika mwisho na inapelekea mtu kutopiga hatua katika biashara yake wala msingi wa biashara yake kukua na kusababisha mtu kuwa kwenye hali ile ile kila siku.
“ Vijana wenzangu nawasihi kuwa na ujasiri na uthubutu wa kufanya mambo mbalimbali katika maeneo yenu ya kazi ikiwemo kuwa na ubunifu katika biashara zenu pamoja na kuhakikisha mnakuwa na kauli nzuri kwa wateja wenu ili kujiongezea wateja zaidi kwenye maeneo yenu ya biashara, kuwa waaminifu kwa wateja wenu hasa kwa bidhaa mnazowauzia na kutokuishi na mteja kimazoea”amesema Msumari.
Katika tukio jingine, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amekabidhi vyeti kwa wahitimu kama kumbukumbu ya mafunzo hayo na kulishukuru Kanisa Huru la Pentekoste nchini kwa kuliomba fursa zingine za mafunzo kama haya zikitokea kuikumbuka wilaya ya Muheza na vijana wajasiriamali wa wilaya ya Muheza.
Kwa upande wake Askofu na Katibu wa jimbo la Tanga FPCT Mch. David Chema amesema lengo la mafunzo haya ni kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kuwakwamua kutoka kwenye hali ngumu ya maisha. Ameendelea kwa kusema kuwa kanisa Huru la Pentekoste nchini limedumu na mradi huu kwa muda wa miaka mitatu nchi nzima likitoa elimu mbalimbali za ujasiriamali kwa vijana kama kuwafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni za maji,batiki na tambi zitakazowasaidia wao kuuza na kujiongezea kipato chao cha kila siku
Ameendelea kuongeza kuwa Kanisa Huru la Pentekoste nchini limekuwa likiratibu shughuli hizi za mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kwa kuwalipa wawezeshaji wa semina hizo pamoja na uendeshaji wa mafunzo hayo kwa ujumla.
Mch.David Chema ameishukuru sana serikali kwa kupata kibali cha kuendesha mafunzo haya wilayani Muheza na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.